Pata taarifa kuu
URUSI- UKRAINE- MAPIGANO

EU mbioni kuihami Ukraine na silaha za kutosha

NAIROBI – Washirika wa nchi ya Ukraine, wapo mbioni kuhakikisha kuwa wanaipa nchi hiyo silaha za kutosha kuisaidia kuendeleza mapigano dhidi ya Urusi, hasa wakati huu mzozo huo ukikaribia mwaka mmoja, ifikapo tarehe 25 mwezi huu.

Umoja wa ulaya unapanga namna ya kuendelea kuisaidia Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi
Umoja wa ulaya unapanga namna ya kuendelea kuisaidia Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi AP - Efrem Lukatsky
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema anatarajia Urusi kuendeleza mashambulio zaidi, huku akimshtumu rais Putin kwa kutokuwa tayari kumaliza vita.

“Ujumbe muhimu ni kuwa hapa hakuna dalili kwamba rais Putin anataka amani.” ameeleza Jens Stoltenberg.

Wawakilishi wa Jumuiya ya Kijeshi ya NATO, wanakutana leo na kesho jijini Brussels kujadiliana msaada zaidi kwa Ukraine.

Uongozi wa Ukraine kwa upande wake umekuwa ukiwataka washirika kuihami na silaha za masafa marefu kuisaidia kupambana na mashabulio yanayotekelezwa na wanajeshi wa Urusi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.