Pata taarifa kuu

Urusi: Mkuu wa Wagner azungumzia malengo ya operesheni ya Urusi Ukraine

Kiongozi wa kampuni binafsi ya kijeshi ya Urusi ya Wagner anaendelea kujaribu kulisaidia jeshi la Urusi kupambana na vikosi vya Ukraine. Katika mahojiano yaliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii, Yevgeny Prigojine ametoa dalili juu ya jinsi anavyoona maendeleo ya operesheni ya Urusi nchini Ukraine, akisisitiza kwamba itachukua miaka kadhaa zaidi kufikia kile anachofikiria kuwa malengo ya operesheni hii.

Kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Wagner Evgeny Prigozhin, akiwa pamoja na Vladimir Putin mnamo 2011.
Kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Wagner Evgeny Prigozhin, akiwa pamoja na Vladimir Putin mnamo 2011. AP - Misha Japaridze
Matangazo ya kibiashara

Evguéni Prigojine anaendelea kuzungumziwa. Ingawa mamlaka ya Urusi haijawahi kueleza hadharani malengo halisi ya kijeshi ya operesheni nchini Ukraine, kiongozi wa kampuni binafsi ya Ulinzi ya Wagner ametoa mwanga kamili kuhusiana na operesheni hiyo. Machoni mwake, anaona kuwa jeshi la Urusi litachukua kati ya mwaka mmoja na nusu na miaka miwili kupata udhibiti kamili wa maeneo ya jamhuri yaliyojitangazia uhuru ya Donetsk na Lugansk.

Ushawishi kwenye uwanja wa kisiasa

Na kama ingefaa kwenda mbali zaidi kuuchukua mji wa Dnipro, kwenye ukingo wa Dnieper, basi hiyo ingehitaji miaka mingine mitatu ya mapigano, anasema Yevgeny Prigojine. Inafahamika kwamba Yevgeny Prigojine aliye na usirikiano wa karibu na Vladimir Putin ni mmoja wa wahamasishaji katika vita nchini Ukraine. Tangu mwezi Februari mwaka uliyopita, hajawahi kujizuia kukosoa amri ya kijeshi ya Urusi. Na kulingana na vyanzo kadhaa, anatumia wanamgambo wa kibinafsi anaowaongoza kupata nguvu fulani kwenye uwanja kisiasa nchini Urusi.

Maneno mazito

Nia ambayo inaelezea misimamo yake na maneno mazito na yenye kebehi. Lakini pia nguvu anazoweka, pamoja na wanamgambo wake, kuuteka mji wa Bakhmout. Ametangaza leo asubuhi kutekwa kwa Krasna Hora, mji ulioko kaskazini mwa Bakhmout.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.