Pata taarifa kuu

Moscow yaishushia lawama Ukraine kwa kushambulia kambi ya wanajeshi wake

Urusi imeishtumu Ukraine kwa kutumia ndege isiyokuwa na rubani, kushambulia kambi yake ya jeshi la anga Kusini mwa taifa lake, na kusababisha vifo vya watu watatu. 

Picha ya setilaiti inaonyesha ndege ya kijeshi katika kambi ya kikosi ch wanahewa ya Engels huko Saratov, Urusi, Desemba 4, 2022.
Picha ya setilaiti inaonyesha ndege ya kijeshi katika kambi ya kikosi ch wanahewa ya Engels huko Saratov, Urusi, Desemba 4, 2022. via REUTERS - MAXAR TECHNOLOGIES
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema, iliangusha ndege hiyo ya Ukraine, baada ya kutekeleza shambulio hilo katika kambi yake ya Engels, na mabaki yake yakawajeruhi, wafanyakazi wake watatu. 

Mapema mwezi huu, Urusi iliishtumu tena Ukraine kwa kutekeleza shambulio kama hili katika kambi yake nyingine ambayo imekuwa ikitumiwa kurusha makombora ndani ya Ukraine. 

Katika hatua nyingine, Ukraine imeitaka Urusi kuondolewa kama mwanachama wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, huku ikiishtumu kwa kursusha makombora zaidia ya 40 katika ardhi yake. 

Wakati hayo yakijiri, Moscow imesema rais Vladimir Putin atazungumza na mwenzake wa China Xi Jinping , wiki hii, wakati huu nchi hiyo inapoendelea kuwekewa vikwazo na nchi za Magharibi kwa sababu ya kuivamia Ukraine. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.