Pata taarifa kuu
UFRANSA-MKASA

Karibia watu 10 wamefariki katika mkasa wa moto mjini Lyon Ufaransa

Nchini Ufaransa, watoto watano ni miongoni mwa watu kumi waliopoteza maisha baada jengo walililokuwa wanaishi kuteketea kwa moto katika mji wa Lyon.

Wazima moto wakiwa katika eneo la mkasa wa moto mjini Lyon
Wazima moto wakiwa katika eneo la mkasa wa moto mjini Lyon AP - Laurent Cipriani
Matangazo ya kibiashara

Watu wengine 14 walijeruhiwa katika mkasa hao uliotokea katika mtaa wa Vaulx-en-Velin, Kaskazini mwa mji huo.

Gerald Darmanin, Waziri wa Mambo ya ndani nchini Ufaransa anasema kuwa tukio hilo ni la kusikitisha.

Tunasikitika kwa kutokea kwa mauaji hayo. Hatufahamu kilichosabisha moto huo, lakini tumeanza uchunguzi wa haraka.” amesema Gerald Darmanin.

Tayari uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha mkasa huo, mamlaka katika êneo hilo zikieleza kuwa ni mapema kutoa taarifa kamili kuhusu tukio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.