Pata taarifa kuu

Ukraine: Urusi yafanya mashambulizi ya angani Kherson, Ukraine yapiga Melitopol

Watu wawili wameuawa na wengine watano kujeruhiwa katika mashambulizi ya mabomu ya Urusi yaliyolenga jimbo la Kherson kusini mwa Ukraine Siku ya Jumapili, Desemba 11, amesema gavana wa jimbo hilo, Yaroslav Yanushevich. Hata hivyo, kwa mujibu wa ushuhuda rasmi unaounga mkono Urusi, vikosi vya Ukraine vilishambulia jioni mji wa Melitopol (kusini mwa Ukraine).

Mkazi akitembea baada ya uharibifu katika jimbo la Kherson, Desemba 7, 2022.
Mkazi akitembea baada ya uharibifu katika jimbo la Kherson, Desemba 7, 2022. REUTERS - STAFF
Matangazo ya kibiashara

"Adui ameshambulia tena maeneo ya makazi ya Kherson," Gavana Yaroslav Yanushevich amesema kwenye ukurasa wake wa Telegram, akisema jeshi la Urusi limeshambulia hospitali ya wazazi, mkahawa na jengo la ghorofa. "Jana usiku, watu wawili waliuawa kwa mashambulizi ya angani ya Urusi" katika jimbo hilo, gavana amesema, akiongeza kuwa umeme umerejeshwa "karibu 90%" katika jiji lenyewe na mazingira yake.

'Mashambulizi 45'

Ameongeza kuwa watu wengine watano wamejeruhiwa kwa viwango tofauti katika "mashambulizi 45" ambayo yalilenga eneo hilo kwa mizinga. Mji wa Kherson ulitekwa tena mwezi Novemba na vikosi vya Ukraine wakati wa kujibu mashambulizi, ambayo yalisababisha kuondolewa kwa majeshi ya Urusi ambayo yalivuka hadi ukingo wa kushoto wa Mto Dnieper. Kabla ya kurudi nyuma mnamo mwezi Novemba, vikosi vya Urusi viliharibu miundombinu ya msingi ya jiji na tangu wakati huo wameshambulia Kherson mara kwa mara.

Katika mji wa Bahari Nyeusi wa Odessa, kukatwa kwa umeme wa dharura kuliendelea kufuatia mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Urusi, msemaji utawala wa jimbo Sergiy Bratchuk amesema siku ya Jumapili (tarehe 11 Desemba). Mamlaka pia imesema "kukatizwa kwa usambazaji wa maji" kumetokea kutokana na kukatika kwa umeme katika sehemu za jiji.

Siku ya Jumamosi, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema zaidi ya watu milioni 1.5 waliachwa bila umemea katika eneo la Odessa baada ya mashambulizi ya Urusi kwa kutumia ndege zisizo na rubani za Iran.

Himars kwenye Melitopol?

Kwa mujibu wa Yevgeny Balitsky, kiongozi aliyeteuliwa na Urusi wa eneo la Zaporizhia, vikosi vya Ukraine vilitumia makombora ya masafa marefu ya Marekani ya Himars kushambulia Melitopol mwendo wa saa tisa alasiri Jumamosi Desemba 10. Shambulio hilo, amesema, liliharibu "kituo cha burudani" nje kidogo ya mji, na kuua watu wawili na kujeruhi wengine kumi. 

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.