Pata taarifa kuu

Ukraine yakaribisha wito wa EU wa kuundwa kwa mahakama maalum kwa 'uhalifu wa Urusi'

Ofisi ya rais wa Ukraine siku ya Jumatano imekaribisha pendekezo la Umoja wa Ulaya la kufanyia kazi kuundwa kwa mahakama maalum ya kwa kushughulikia "uhalifu wa Urusi" nchini Ukraine. 

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akihutubia kwa njia ya video kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York mnamo Septemba 21, 2022.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akihutubia kwa njia ya video kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York mnamo Septemba 21, 2022. AFP - ANGELA WEISS
Matangazo ya kibiashara

"Hivi ndivyo tumekuwa tukipendekeza kwa muda mrefu", amesema kwenye Telegraph mkurugenzi kwenye ofisi yarais wa Ukraine, Andriï Iermak, baada ya tangazo la Tume ya Ulaya kutaka kujikita katika uundaji wa mahakama kama hiyo na kuanzisha taratibu za kutumia mali za Urusi zilizozuiliwa katika ujenzi wa Ukraine.

Umoja wa Ulaya unataka kuundwa kwa mahakama maalum ya kuchunguza na kuhukumu uwezekano wa uhalifu wa kivita uliofanywa nchini Ukraine na Urusi. Kwa upande wake, Ukraine siku ya Jumanne ilitoa wito kwa nchi wanachama wa NATO wanaokutana Bucharest kuharakisha utoaji wa silaha na vifaa vya umeme ili kusaidia nchi hiyo kukabiliana na uharibifu kwa miundombinu yake ya nishati na mashambulizi ya angani ya Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.