Pata taarifa kuu

Uingereza: Waziri Mkuu Liz Truss ajiuzulu

Liz Truss ametangaza kujiuzulu kama waziri mkuu wa Uingereza baada ya kushikilia nafasi hiyo kwa siku 45 pekee. Bi Truss amesema atasalia kwenye wadhifa huo hadi mrithi atakapochukua rasmi wadhifa wa kiongozi wa chama na atateuliwa kuwa waziri mkuu na Mfalme Charles III.

Waziri Mkuu wa Uingereza Liz Truss huko London, Alhamisi, Oktoba 20, 2022.
Waziri Mkuu wa Uingereza Liz Truss huko London, Alhamisi, Oktoba 20, 2022. AP - Alberto Pezzali
Matangazo ya kibiashara

Kwa kulazimishwa katika mfululizo wa mabadiliko ya ahadi zake za kampeni, Waziri Mkuu wa Uingereza Liz Truss ilimbidi hasa kumbadilisha waziri wa fedha baada ya bajeti iliyowasilishwa mwishoni mwa mwezi Septemba kusababisha hofu katika masoko ya fedha.

"Kwa kuzingatia hali hiyo, siwezi kukamilisha muhula wangu baada ya kupewa nafasi ya kuwania kwenye wadhifa huo na Chama cha Conservative", ametangaza Liz Truss nje ya Mtaa wa Downing. Amebainisha kuwa kura mpya ya ndani itafanyika katika walio wengi "ifikapo wiki ijayo" kuchukua nafasi yake.

Katika hotuba nje ya Mtaa wa Downing, Bi Truss alisema Chama cha Conservative kilimchagua kwa jukumu la kupunguza ushuru na kukuza ukuaji wa uchumi.

Kiongozi wa upinzani nchini Uingereza kutoka chama cha Labor, Keir Starmer, ametaka uchaguzi mkuu ufanyike "sasa".

Shinikizo lilikuwa linaongezeka kwa Liz Truss. Waziri Mkuu wa Uingereza, ambaye alikuwa mamlakani kwa wiki 6, na ambaye alipata siku "ngumu" siku ya Jumatano kufuatia kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na kuripotiwa mvutano mkali katika Bunge Jumatano jioni.

Awali msemaji wa Waziri Mkuu alihakikisha kwamba hakuwa na nia ya kuachia ngazi. Lakini leo asubuhi, alikutana na mbunge anayesimamia Kamati yenye nguvu ya 1922 inayosimamia utaratibu wandani wa chama cha Conservative. Mkutano ambao unaonekana kubadili mazingira yaliyopangwa na Waziri Mkuu. Kwa hivyo, chama cha Conservative kinaanza tena uchaguzi wa ndani ili kupata kiongozi mpya, wa tano katika miaka sita.

Liz Truss anakuwa Waziri Mkuu aliyehudumu kwa muda mfupi zaidi, akiwa na siku 45 tu madarakani tangu alipomrithi Boris Johnson mnamo Septemba 6, 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.