Pata taarifa kuu

Umoja wa Ulaya kupiga marufuku visa kwa Warusi wote

Marufuku ya visa kwa Warusi wote kuiadhibu Moscow kwa vita vya Ukraine itajadiliwa mwishoni mwa mwezi wa Agosti na Umoja wa Ulaya. Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Jan Lipavsky, ambaye nchi yake ni mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Ulaya, EU, amebainisha.

"Marufuku kamili ya  nchi zote wanachama wa EU dhidi ya visa vya Urusi inaweza kuwa vikwazo vingine bora dhidi ya Urusi," amebainisha mkuu wa diplomasia ya Jamhuri ya Czech.
"Marufuku kamili ya nchi zote wanachama wa EU dhidi ya visa vya Urusi inaweza kuwa vikwazo vingine bora dhidi ya Urusi," amebainisha mkuu wa diplomasia ya Jamhuri ya Czech. REUTERS - Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii, iliyokuwa ikiombwa na mamlaka ya Ukraine, imesababisha mgawanyiko ndani ya Umoja wa Ulaya. Vikwazo vya Ulaya lazima vipitishwe kwa kauli moja na nchi Ishirini na Saba, wanachama wa umoja huo. "Marufuku kamili ya visa vya Urusi na mataifa yote wanachama wa EU inaweza kuwa vikwazo vingine vyenye ufanisi dhidi ya Urusi," amesema Jan Lipavsky. Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech atazungumza na wenzake wakati wa mkutano usio rasmi mwishoni mwa mwezi wa Agosti huko Prague. "Katika kipindi hiki cha uchokozi wa Urusi, ambacho Kremlin inaendelea kuzidisha, haitaweza kuwa suala la utalii kama kawaida kwa raia wa Urusi," amesema.

Hata hivyo waziri huyo wa Jamhuri ya Czech atamshawishi mkuu wa diplomasia ya Ulaya, Mhispania Josep Borrell, ambaye ni mwenyekiti wa Mabaraza ya Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi. Mapendekezo ya vikwazo ni mojawapo ya haki zake: "Hatuwezi kwa sasa kuzuia watu wenye visa kutoka nchi nyingine kuingia katika eneo la Schengen. Tunatafuta chaguzi,” Waziri Mkuu wa Estonia Kaja Kallas alisisitiza hivi majuzi, akiunga mkono marufuku ya jumla.

Ufini pia inatetea uamuzi wa Ulaya, kwani sheria za nchi hiyo haziruhusu marufuku kamili ya visa kwa kuzingatia utaifa. Nchi hii muhimu ya usafiri kwa Warusi, inataka kupunguza visa vya watalii, Waziri wa Mambo ya Nje Pekka Haavisto alisema mapema mwezi Agosti.

Haja ya kuwalinda wapinzani na waandishi wa habari

Tume haifichi kusita kwake kuhusu hatua ambayo itawaadhibu raia wote wa Urusi na inasisitiza juu ya hitaji la kuwalinda wapinzani, waandishi wa habari na familia: "Nchi Wanachama zina nafasi kubwa ya kutoa visa kwa kukaa kwa muda mfupi na huchunguza maombi kwa kila mtu kwa msingi wa sifa zao, "amekumbusha mmoja wa wasemaji wake.

"Warusi wanaunga mkono vita kwa kiasi kikubwa, wanapongeza mashambulio ya makombora kwenye miji ya Ukraine na mauaji dhidi ya Waukraine. Kwa hivyo waache watalii wa Urusi wafurahie Urusi,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kouleba amesema katika ujumbe kwenye Twitter.

Jamhuri ya Czech iliacha kutoa visa kwa Warusi mnamo Februari 25, siku moja baada ya Urusi kuivamia Ukraine. EU imepitisha seti sita za vikwazo dhidi ya Moscow, ikiwa ni pamoja na kusitisha ununuzi wake wa makaa ya mawe na mafuta. Pia imeongeza zaidi ya Warusi elfu moja, ikiwa ni pamoja na rais Vladimir Putin na viongozi wengi, kwenye orodha yake nyeusi ya wale waliopigwa marufuku kuingia nchini humo na imezuia utoaji wa visa vya muda mfupi kwa maafisa wenye uhusiano na serikali tangu mwisho wa mwezi wa Februari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.