Pata taarifa kuu
MAFURIKO KENTUCKY MAREKANI

Kentucky: 19-wafa katika mafuriko kwenye eneo la Appalachia Marekani

Karibia watu 19 wameripotiwa kufariki kutokana na mafuriko yaliosababishwa na mvua kubwa katika eneo la Appalachia kaskazini mwa jimbo la Kentucky nchini Marekani – Hili likitajwa kuwa janga mbaya zaidi kuwahi likumbuma eneo hilo.

Makazi ya raia katika jimbo la Kentucky, Julai 29  2022.
Makazi ya raia katika jimbo la Kentucky, Julai 29 2022. Getty Images via AFP - MICHAEL SWENSEN
Matangazo ya kibiashara

Gavana wa jimbo la Kentucky Andy Beshear amesema kuwa huenda idadi ya waliofariki ikaendelea kuongezeka.

Kiongozi huyo aidha ameongeza kuwa mamia ya makazi ya raia na maeneo ya biashara yamejaa maji.

Rais wa Marekani Joe Biden ametaja mafuriko hayo kama janga kubwa ambapo ameamuru usaidizi wa haraka kwa walioathiriwa.

Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na watoto sita akiwemo mtoto wa mwaka moja.

Wanasayansi wameeleza kuwa mabadiliko ya tabia nchi yamechangia kutokea kwa matukio kama hili la mafuriko ya Kentucky.

Karibia watu 33,000 katika eneo hilo wanakabiliwa na tishio la umasikini, umeme umesemakana kukatika kutokana na mafuriko hayo, barabara zikiwa hazipitiki baada  ya kuzibwa na mapromoko ya udongo.

Japokuwa eneo hilo limekuwa likishuhudia mafuriko, mamlaka katika mji huo zimedhibitisha kuwa hayajawahi fikia kiwango hiki.

Watu wametakiwa kuhamia katika maeneo salama wakati huu mvua ikitarajiwa kuendelea kunyesha wiki ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.