Pata taarifa kuu

Jeshi la Ukraine lapewa amri ya kuondoka katika mji wa Sievierodonetsk

Katika siku ya 121 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine , vikosi vya Ukraine vimepewa amri ya kuondoka katika jiji la Sievierodonetsk linalokumbwa na mashambulizi ya jeshi la Urusi katika eneo hili la jimbo la Donbass.

Wanajeshi wa Ukraine wakipiga doria katika mji wa Sievierodonetsk.
Wanajeshi wa Ukraine wakipiga doria katika mji wa Sievierodonetsk. © Oleksandr Ratushniak/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kujaribu kufanya upinzani dhidi ya kusonga mbele kwa  Urusi, jeshi la Urusi limeamriwa kuondoka jiji la Sievierodonetsk.

Wakati huo huo Huko Brussels, makao makuu ya Umoja wa Ulaya, nchi Ishirini na Saba wanacxhama wa umoja huo zilizipa Ukraine na Moldova hadhi ya kuwania kuwa wanachama wa Umoja wa Ulaya siku ya Alhamisi, ikia ni hatua muhimu.

Mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya siku ya Alhamisi huko Brussels utafuatiwa katika siku hizi na mikutano ya G7 na NATO. Suala la msaada wa kifedha na kijeshi kwa Kyiv litagubika vikao hivi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.