Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Wakazi wa Donbass wachoka na vita lakini ni wastahimilivu

Mkoa wa Donbass sasa unakabiliwa na mashambulizi ya Urusi kila wakati. Baadhi ya raia iwamelazimika kuyatoroka makazi yao, huku Waukraine wengine wameamua kubaki licha ya shida zinazowakabili kila siku.

Wafanyakazi waliostaafu wanakuja kwenye dirisha la gari la Poste kuchukua pensheni yao huko Starodubivka, mashariki mwa Sloviansk, mnamo Juni 15, 2022.
Wafanyakazi waliostaafu wanakuja kwenye dirisha la gari la Poste kuchukua pensheni yao huko Starodubivka, mashariki mwa Sloviansk, mnamo Juni 15, 2022. © Cléa Broadhurst
Matangazo ya kibiashara

Maisha ya kila siku ya wakazi wa Donbass ni magumu kila kukicha: kunaripotiwa uhaba  wa vifaa mbalimbali na chakula na mashambulizi ya Urusi yanakaribia. Karibu mita mia moja kutoka uwanja wa vita, katika kijiji cha Starodubivka, watu wanakabiliwa na uhaba wa maji. “Tuna kisima kimoja tu kwa kijiji chetu kizima. Hakuna maji tena, "anasema Kateryna, mwanamke mzee mwenye umri wa miaka sitini ambaye alikuja kwa miguu kufanya shughuli katika duka moja.

"Hali ni nzito. Na hatuna umeme tena. Kwa hivyo tunaweka chakula chetu katika chumba cha chini cha ardhi. Tutaishi hapa bila kuwa umeme. Tutaendelea kufanya nini hapa? Ninachoogopa ni msimu wa baridi ambao unaingia, lakini nilizaliwa hapa na nitafia hapa. »

Tangu kuondoka kwao katika eneo la Kyiv na kaskazini-magharibi mwa nchi, wanajeshi wa Urusi wameelekeza juhudi zao mashariki mwa nchi kuchukua udhibiti wa jimbo la Donbass. "Katika eneo la Donetsk, wanajeshi wa Urusi wana silaha nyingi zaidi, vifaru, mashine za vita," anasema Maxime, mwanajeshi ambaye mwanzoni mwa vita alikuwa upande wa kusini mwa nchi lakini sasa yuko karibu na Bakhmut, katikati ya jimbo la Donbass.

"Ikiwa tutalinganisha mapigano katika mikoa ya Kherson na Donetsk, huko Kherson tulikuwa likizoni. Katika mkoa wa Kherson, tulikabiliana mara chache na jeshi la Urusi. Lakini huko Donetsk, unapofyatua risasi mara moja, wanajeshi wa Urusi wanafyatua risasui mara kumi zaidi. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.