Pata taarifa kuu

Ukraine: Runinga ya Urusi yaonyesha wanajeshi wawili wa Kimarekani waliotoweka

Katika siku ya 115 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumamosi Juni 18, Marekani imejibu kwa tahadhari baada ya televisheni ya Urusi ya RT kurusha hewani video zinazoonyesha wanajeshi wawili wa Marekani waliokamatwa. Siku ya Ijumaa, Tume ya Ulaya ilipendekeza kukubali Ukraine kuwa kupewa nafasi ya kuwa mwanachama waUmoja wa Ulaya, EU.

Alexander Drueke, veterani wa jeshi la Marekani, alikuwa amekwenda kupigana nchini Ukraine dhidi ya jeshi la Urusi. Siku ya Ijumaa, Juni 17, 2022Televisheni ya serikali ya Urusi ilirusha hewani picha zinazomuonyesha yeye na mwanajeshi mwingine wa Marekani, Andy Huynh. Wote wawili wanashikiliwa na jeshi la Urusi.
Alexander Drueke, veterani wa jeshi la Marekani, alikuwa amekwenda kupigana nchini Ukraine dhidi ya jeshi la Urusi. Siku ya Ijumaa, Juni 17, 2022Televisheni ya serikali ya Urusi ilirusha hewani picha zinazomuonyesha yeye na mwanajeshi mwingine wa Marekani, Andy Huynh. Wote wawili wanashikiliwa na jeshi la Urusi. AP - Lois "Bunny" Drueke
Matangazo ya kibiashara

Runinga ya serikaliya Urusi imerusha hewani video za maveterani wawili wa jeshi la Marekani, Alexander Drueke na Andy Huynh, ambao waliondoka kwenda kupigana nchini Ukraine dhidi ya jeshi la Urusi. Ingawa hawakuwa wamesikika kwa siku kadhaa, wameonekana kwenye video hizo wakiwa wafungwa wa jeshi la Urusi karibu na mji wa Kharkiv.

Tume ya Ulaya ilisema siku ya Ijumaa kuwa inapendelea kutoa hadhi ya Ukraine kuwa mwanachama wa EU. Ni wakati wa mkutano wa kilele wa Juni 23 na 24 huko Madrid ambapo nchi Ishirini na Saba wanachama wa umoja huo wataamua ikiwa itaipa Ukraine hadhi hii rasmi, ambayo itafungua mazungumzo ambayo yanaweza kudumu kwa miaka kadhaa.

Katika ziara yao nchini Ukraine siku ya Alhamisi, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi, pamoja na mwenzao wa Romania, walisema wako tayari kuipa Ukraine "mara moja" hadhi ya kuwa mgombea kwa kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Hali ya kibinadamu huko Donbass "ni ya kutisha sana", Umoja wa Mataifa umesema, wakati mapigano kati ya majeshi ya Ukraine na Urusi yakiendelea kupamba moto mashariki mwa nchi hiyo, hasa katika eneo la Sievierodonetsk.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.