Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI-EU

Umoja wa Ulaya kutoa uamuzi iwapo Ukraine inaweza kuwa mwanachama

Umoja wa Ulaya sasa inasema, itatoa mtazamo wake wiki ijayo, iwapo Ukraine inaweza kuwa mwanachama wake mpya.

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Ulaya  Ursula von der Leyen, akiwa na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, jijni Kiev Juni 11 2022
Mkuu wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, akiwa na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, jijni Kiev Juni 11 2022 AP - Natacha Pisarenko
Matangazo ya kibiashara

Hii imethibitishwa na Ursula von der Leyen Mkuu wa Tume ya Umoja wa Ulaya, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jijini Kiev na kufanya mazungumzo na rais Volodymyr Zelensky.

"Tunamalizia thathmini yetu, kabla ya kufanya maamuzi wiki ijayo,” alisema.

Wakati hayo yakijiri, rais Zelensky anasema wanajeshi wa nchi yake wanaendelea kukabiliana katika vita vigumu, hasa katika jimbo la Mashariki la Donbas ambalo wanajeshi wa Urusi wanaendeleza mashambulio.

Aidha, Zelensky amesema licha ya vita kuwa vigumu, wanajeshi wa Ukraine wanafanya kile kinachowezekana, kuhakikisha kuwa wanawarudisha nyuma wanajeshi kutoka Urusi.

Siku ya Jumamosi, mapigano makali yameendelea kuripotiwa katika mji wa Severodonetsk, huku Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ikisema pande zote zinapata hasara kubwa.

Gavana wa jimbo la Mykolaiv Vitaly Kim,anasema wanajeshi wa Ukraine wanaokena kushiwa silaha, na anazitaka nchi za Magharibi kuleta haraka slaha zaidia hasa makombora ya masafa marefu, ili kuendelea kupâmbana na Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.