Pata taarifa kuu

Ukraine: Urusi yatafuta askari dhaifu katika ulinzi wa Ukraine karibu na Seversky Donets

Urusi inatafuta maafisa dhaifu katika ulinzi wa Ukraine karibu na Mto Severski Donets mashariki mwa Ukraine, msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Ukraine Oleksandr Motuzyanyk amesema leo Ijumaa.

Hali nchini Ukraine, Juni 3, 2022.
Hali nchini Ukraine, Juni 3, 2022. © FMM
Matangazo ya kibiashara

Oleksandr Motuzyanyk amedai kwenye televisheni ya taifa kwamba vikosi vya Urusi havijakata tamaa katika majaribio yao ya kuanzisha operesheni za mashambulizi katika eneo hilo.

 

Ikiwa Urusi itaiteka miji ya Sievierodonetsk na Lyssychansk kwenye Mto Seversky Donets, itashikilia Luhansk yote, mojawapo ya majimbo mawili ya Donbass ambayo Moscow inadai kwa niaba ya wanaotaka kujitenga.

Hayo yanajiri wakati Rais wa Ukraine ametoa wito wa kutengwa kwa Urusi katika Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), ambayo inakabiliwa na shutuma za Kyiv za kuzuia na wizi wa nafaka za Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.