Pata taarifa kuu

Ukraine: Ulaya yashindwa kuafikiana juu ya mtazamo wa kuchukua dhidi ya Urusi

Katika siku ya 107 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Ijumaa hii, Juni 10, fuata moja kwa moja habari za hivi punde kuhusu mzozo huo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Berlin (Ujerumani), Mei 9, 2022
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Berlin (Ujerumani), Mei 9, 2022 © EMMANUELE CONTINI / NURPHOTO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wa Ukraine wanapambana dhidi ya vikosi vya Urusi huko Sievierodonetsk moja ya "vita ngumu zaidi" tangu kuanza kwa vita kupinga vikosi vya Urusi ambavyo sasa vinadhibiti sehemu kubwa ya mji huu wa kimkakati wa mashariki ambapo, kulingana na Rais Volodymyr Zelensky, "hatma" ya eneo la Donbass iko hatarini.

"Hadi wanajeshi 100 wa Ukraine" wanauawa na "500 kujeruhiwa kila siku" katika vita na jeshi la Urusi, Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Oleksiï Reznikov alisema siku ya Alhamisi.

Rais wa Ukraine ametoa wito wa kutengwa kwa Urusi katika Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), ambayo inakabiliwa na shutuma za Kyiv za kuzuia na wizi wa nafaka za Ukraine.

Waingereza wawili na raia wa Morocco waliochukuliwa kama wafungwa mashariki mwa Ukraine, ambapo walikuwa wakipigana kwa upande wa Kyiv, walihukumiwa na mamlaka ya wanamgambo waliojitenda wanaounga mkono Urusi ya Donetsk adhabu  ya kifo, mashirika ya habari ya Urusi yalitangaza tarehe 8 Juni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.