Pata taarifa kuu

Miili kadhaa yagunduliwa mjini Mariupol, wakati mzozo wa chakula ukizidisha hofu

Serikali nchini Ukraine imesema miili zaidi ya watu imepatikana kutoka vifusi vya majengo yaliyoharibiwa kwa vita mjini Mariupol, wakati huu mzozo wa chakula ukizidisha hofu duniani kutokana na nchi hiyo kushindwa kusafirisha nafaka kupitia bandari zilizofungwa.

Katika moja ya makaburi ya jiji la Mariupol, Juni 2, 2022.
Katika moja ya makaburi ya jiji la Mariupol, Juni 2, 2022. AFP - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini Ukraine inakadiria kuwa, raia wapatao 21,000 wameuawa mjini Mariupol tangu vikosi vya Urusi vilipoanzisha mashambulizi ya wiki kadhaa mjini humo.

Athari ya vita hivyo inaonekana pia katika sehemu nyengine duniani kwa sababu shehena za nafaka kutoka Ukraine zimezuiwa kuondoka nchini humo, hivyo basi kusababisha kupanda maradufu kwa bei za vyakula.

Kulingana na msaidizi wa meya katika mji Mariupol unaodhibitiwa na Urusi Petro Andryushchenko, wafanyikazi wanaochimba vifusi wanapata miili 50 hadi 100 kwa siku. Msaidizi huyo wa meya ameandika kupitia mtandao wa Telegram kuwa, miili hiyo inapelekwa katika kile alichokiita "msafara wa kifo usio na kikomo" hadi vyumba vya kuhifadhia maiti na maeneo mengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.