Pata taarifa kuu

Mapigano yarindima Sievierodonetsk; Mashariki mwa Ukraine

Katika siku ya 104 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumanne, Juni 7, mapigano yanandelea kwa lengo la kudhibiti eneo la Sievierodonetsk, mashariki mwa Ukraine ambapo hali inabadilika "saa hadi saa", kulingana na Kyiv.

Wanajeshi wa Ukraine kwakiwa karibu na uwana wa vita mkoa wa Donetsk mnamo Juni 6, 2022.
Wanajeshi wa Ukraine kwakiwa karibu na uwana wa vita mkoa wa Donetsk mnamo Juni 6, 2022. AP - Bernat Armangue
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya Ukraine vinavyolinda jiji la Sievierodonetsk, Mashariki mwa Ukraine, "vinajizatiti vilivyo" licha ya mashambulizi ya askari kutoka Moscow, lakini wanajeshi wa Urusi ni "wengi zaidi na wana silaha kali na zenye uwezo zaidi", alisema Jumatatu rais wa Ukraine. Gavana wa eneo hilo alikuwa ameashiria hapo awali kwamba hali "ni mbaya zaidi" kwa jeshi la Ukraine katika jiji hili la Donbass na vile vile karibu na mji wa Lysytchansk.

Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken siku ya Jumatatu aliishutumu Moscow kwa "usindikaji" katika kuondoa vikwazo vya kimataifa kwa kuzuia mauzo ya ngano kutoka Ukraine. Pia alidai kuwa na habaruiza "kuaminika" kwamba Urusi inaiba tani za nafaka, ili kuziuza kwa faida yake yenyewe.

Nchi za Ulaya zinazopatikana karibu na Serbia zilifunga anga zao Jumatatu kwa ndege ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov, ambayo ilitarajiwa kutua huko Belgrade siku ya Jumatatu. Uamuzi ambao ulisababisha Moscow kupandwa na hasira, na kubaini kwamba uamuzi huo unachochea uhasama.

Marekani na Ulaya wanaitaka Urusi kukomesha madai ya unyanyasaji wa kingono uliofanywa na jeshi lake na washirika wake nchini Ukraine, huku Moscow ikikashifu shutuma zisizo na msingi wakati wa mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.