Pata taarifa kuu

Ukraine: Volodymyr Zelensky kutembelea wanajeshi wake 'kunatoa matumaini'

Katika siku ya 103 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumatatu Juni 6, Kyiv inadai kutwaa tena "nusu" ya eneo la Sievierodonetsk na kusonga mbele katika mji huu wa Donbass unaokumbwa na mashambulizi makali kutoka kwa vikosi vya Urusi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwatia moyo wanajeshi wake katikauwanja wa Vithuko Donetsk mnamo Juni 5, 2022.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwatia moyo wanajeshi wake katikauwanja wa Vithuko Donetsk mnamo Juni 5, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitembelea wanajeshi wake walio kwenye uwanja wa vita mashariki mwa nchi hiyo siku ya Jumapili, ambapo alizungumza na wanajeshi, amebaini kwenye video. Rais wa Ukraine pia alitembelea mji wa Zaporizhya ambapo alikutana na wakaazi wa Mariupol.

Mji mkuu wa Ukraine, Kyiv , ambao umekuwa umeanza tena kushuhudia hali ya utulivu, ulikumbwa na mashambulizi kadhaa ya Urusi alfajiri siku ya Jumapili, ikiwa ni mashambulizi ya kwanza tangu mwishoni mwa mwezi wa Aprili.

Siku ya Jumapili jeshi la Ukraine lilisema kwamba limerejesha kwenye himaya yake "nusu" ya eneola Sievierodonetsk na kusonga mbele katika mji huu muhimu wa Donbass unaokumbwa na mashambulizi makali kutoka kwa vikosi vya Urusi.

Hayo yanajiri wakati Ukraine haitashiriki katika michuano ya soka ya Kombe la Dunia. Timu ya taifa ilipoteza Jumapili usiku huko Cardiff 1-0 dhidi ya Wales kwenye fainali ya mchujo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.