Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI-MAREKANI

Marekani kutuma maroketi yenye uwezo mkubwa nchini Ukraine

Marekani itatuma makombora na maroketi  yenye uwezo mkubwa nchini Ukraine, kuisaidia kupambana na Urusi ambayo inaendelea kuishambulia nchi hiyo.

Silaha za kivita
Silaha za kivita REUTERS/Valentyn Ogirenko
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani amenukuliwa na Gazeti la la The New York Times, akisema mitambo hiyo itaisadia Ukriane kulenga maeneo muhimu yanayotumiwa na wanajeshi wa Urusi, kuendeleza mashambulizi nchini Ukraine.

Afisa wa juu wa serikali ya Marekani naye, amesema makombora hayo yana uwezo wa kufikia mbali na yatalisaidia jeshi la Ukraine kusambaratisha mipango ya wanajeshiwa Urusi.

Siku ya Jumatano Marekani inatarajiwa kutanagza msaada zaidi wa vifaa vya kijeshi kwa Ukraine, vilivyo na thamani ya Dola Milioni 700, yakiwemo magari ya kijeshi na ndege.

Katika hatua nyingine, rais Volodymyr Zelenskyy amesema vikosi vyake vinaendelea kudhibiti baadhi ya maeneo ya jimbo la Kharkiv.

Naye kiongozi wa mashtaka wa Ukraine Iryna Venediktova amesema, visa zaidi ya Elfu 15 vya uhalifu wa kivita, vimreripotiwa katika nchi yake na washukiwa zaidia ya 600 wametambuliwa wakiwemo wanasiasa, viongozi wakuu wa jeshi wanaoshiriliana na Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.