Pata taarifa kuu

Urusi: Rekodi ya mapato ya hidrokaboni kwa sehemu hufadhili vita nchini Ukraine

Wakati nchi ishirini na saba bado hazijaweza kupata mwafaka juu ya mradi wa vikwazo vya pamoja kwa mafuta ya Urusi - kwa sababu ya kuzuiwa kwake na Hungary - Urusi bado inanufaika kwa mapato ya rekodi kutoka kwa mauzo yake ya hidrokaboni kwa kiasi kikubwa bila vikwazo vilivyowekwa baada ya uvamizi wake nchini Ukraine.

Mwaka huu, mauzo ya nje ya hydrokarboni yataingizia Urusi Ruble bilioni 1000, au euro bilioni 13 milioni 700, sehemu ya pesa hii itawezesha Moscow kuendelea na mashambulizi yake nchini Ukraine.
Mwaka huu, mauzo ya nje ya hydrokarboni yataingizia Urusi Ruble bilioni 1000, au euro bilioni 13 milioni 700, sehemu ya pesa hii itawezesha Moscow kuendelea na mashambulizi yake nchini Ukraine. © REUTERS/Sergei Karpukhin
Matangazo ya kibiashara

Mwaka huu, mauzo ya nje ya hidrokaboni yataiwezesha Urusi kunufaika kwa Rubles bilioni 1,000, au euro bilioni 13.7. Sehemu ya fedha hizi itawezesha Moscow kuendelea na mashambulizi yake nchini Ukraine. Tangazo hilo limetolewa na Waziri wa Fedha wa Urusi Anton Silouanov.

Akiba yashuka

Kabla ya vita, mauzo ya mafuta na gesi yalisaidia kujaza akiba ya fedha za kigeni za Benki Kuu ya Urusi. Akiba hizi, nguzo ya uchumi wa Urusi, zilifikia zaidi ya dola bilioni 643. Lakini tangu wakati huo, sehemu ya hifadhi hizi zilikuwa zimezuiwa nje ya nchi, na kilichobaki kinaendelea kupungua.

Hata hivyo, Moscow inahitaji rasilimali hizi ili kusaidia fedha zake, Ruble, lakini pia kulipa gharama zake. Mwaka huu, pesa zinazotokana na mauzo ya nje ya hydrokarboni zitatutumika kikamilifu, waziri amesema.

Mapato kutoka kwa mafuta, bidhaa zilizosafishwa na gesi huleta fedha nyingi kwa Urusi: Ni zaidi ya theluthi moja ya bajeti yake mnamo mwaka 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.