Pata taarifa kuu

Ukraine: Urusi yathibitisha kutekwa kwa eneo muhimu la Lyman, Donbass

Katika siku ya 94 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumamosi Mei 28, jeshi la Urusi limezidisha mashambulizi yake huko Donbass, na kushinikiza vikosi vya Ukraine kupanga namna ya kujiondoa baadhi ya maeneo ya vita katika jimbo hili la mashariki mwa nchi.

Picha ya setilaiti inaonyesha majengo yaliyoharibiwa na gari la kijeshi kwenye barabara ya Lyman, Mei 25, 2022.
Picha ya setilaiti inaonyesha majengo yaliyoharibiwa na gari la kijeshi kwenye barabara ya Lyman, Mei 25, 2022. via REUTERS - MAXAR TECHNOLOGIES
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Urusi limethibitisha Jumamosi kupata ushindi wa eneo la Lyman, mashariki mwa Ukraine, eneo muhimu la Donbass, ambalo baadhi ya maeneo yake yamedhibitiwa na kikosi chawapiganaji waliojitenga tangu mwaka 2014. Mafanikio haya yamefungua njia ya vituo vya kikanda vya Sloviansk, kisha Kramatorsk, huku ikiwawezesha kukaribia kuzingira eneo la kimkakati linaloundwa na miji ya Sievierodonetsk na Lyssytchansk.

Tawi la Moscow la Kanisa la Kiorthodoksi la Ukraine limeamua kukata uhusiano na mamlaka ya kiroho ya Urusi, ambayo inamuunga mkono Rais wa Urusi Vladimir Putin, ikiwa ni uamuzi wa kihistoria.

Ripoti huru ya kwanza inaonya kuhusu "hatari kubwa na inayokaribia" ya mauaji ya kimbari nchini Ukraine. ripoti hii ambayo metiwa saini na wasomi na wataalam zaidi ya thelathini, inaishutumu Urusi kwa kukiuka vifungu kadhaa vya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari, kwa msingi wa tuhuma hizi kwenye mifano kadhaa ya mauaji ya raia wengi na uhalifu mwingi.

Zaidi ya raia 4,000 wameuawa nchini Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi mnamo Februari 24, unasema Umoja wa Mataifa, ambao unaonya kuwa kuna uwezekano mkubwa wa idadi ya wakimbizi kuwa kubwa zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.