Pata taarifa kuu

[Moja kwa moja] Mkutano wa Davos kugubikwa na vita nchini Ukraine

Katika siku ya 89 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumatatu hii, Mei 23, fuata moja kwa moja habari za hivi punde kuhusu mzozo huo.

Jengo la utawala lililoharibiwa huko Azovstal Iron na Steel Works katika jiji la bandari la Mariupol, Ukraine, Mei 22, 2022.
Jengo la utawala lililoharibiwa huko Azovstal Iron na Steel Works katika jiji la bandari la Mariupol, Ukraine, Mei 22, 2022. REUTERS - PAVEL KLIMOV
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Vita na hatari zinazotokana na vita hivyo katika kufufua uchumi wa dunia vitakuwa kiini cha mkutano wa viongiozi wa dunia, ambao wanakutana kuanzia Jumatatu hii huko Davos.

► Sheria ya kijeshi na uhamasishaji wa jumla nchini Ukraine imeongezwa kwa miezi mitatu, hadi Agosti 23.

► Siku ya Jumapili Rais wa Poland Andrzej Duda alisema mjini Kyiv kwamba amedhamiria kufanya kila liwezekanalo kuisaidia Ukraine kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

► Ukraine haitakubali kusitishwa kwa mapigano na Urusi na haitakubali makubaliano yoyote na Moscow yanayohusu kukaliwa kwa moja ya maeneo yake, anasema mshirika wa karibu wa Volodymyr Zelensky. Kwa upande wake, Urusi inasema iko tayari kuanzisha upya mazungumzo hayo.

► Mapigano yanapamba moto huko Donbass, mashariki mwa Ukraine, huku Waziri wa Ulinzi wa Urusi akisema kuwa ushindi wa eneo la Luhansk unakaribia kukamilika. Katika eneo hili, Sievierodonetsk na Lyssytchansk, ambazo sasa zimezingrwa na vikosi vya Urusi, ni ngome ya mwisho ya upinzani wa Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.