Pata taarifa kuu

EU yapanga kukomesha utegemezi wa uagizaji wa mafuta ya Urusi kutoka nje

"Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umevuruga kwa kiasi kikubwa soko la nishati la Ulaya na kimataifa. REPowerEU ni mpango wetu wa kukomesha utegemezi wa Umoja wa Ulaya kwa uagizaji wa mafuta kutoka Urusi. Itatuwezesha kujenga miundombinu mpya na mfumo mpya wa nishati ambao Ulaya inahitaji, " imesema tume ya Ulaya.

Mitambo iliyoharibiwa ya kiwanda cha chuma cha Azovstal katika vita vya Ukraine na Urusi katika jiji la bandari la Mariupol, Ukrainie, Mei 22, 2022. Picha iliyopigwa na ndege isiyo na rubani
Mitambo iliyoharibiwa ya kiwanda cha chuma cha Azovstal katika vita vya Ukraine na Urusi katika jiji la bandari la Mariupol, Ukrainie, Mei 22, 2022. Picha iliyopigwa na ndege isiyo na rubani REUTERS - PAVEL KLIMOV
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Joe Biden alisema mnamo Mei 23 mjini Tokyo kwamba Urusi "lazima ihukumiwe" kwa "unyama wake wa kishenzi nchini Ukraine" katika suala la vikwazo vilivyowekwa na Marekani na washirika wake. "Sio tu kuhusu Ukraine," Biden alisema. Kwa sababu ikiwa "vikwazo havitadumishwa katika mambo mengi, basi hiyo itatuma ishara kwa China kuhusu gharama ya jaribio la kuichukua Taiwan kwa nguvu? alijiuliza.

Wakati huo huo Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel, alikutana na kila upande kwa wakati wake siku ya Jumapili (Mei 22) mjini Brussels, baada ya Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan na Waziri Mkuu wa Armenia, Nikol Pashinyan, kukutana na kukubaliana juu ya umuhimu wa kuendeleza mpango wa amani, kwa mujibu wa Michel.

Charles Michel amendelea kuwa, mawaziri wa mambo ya nje watakutana katika wiki za hivi karibuni kuratibu muendelezo wa majadiliano na marais hao watatu watakutana baina ya Julai na Agosti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.