Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Ufaransa: Emmanuel Macron, ajiandaa kurejea ikulu siku chache zijazo

Emmanuel Macron aliyechaguliwa tena kuwa rais wa Ufaransa kwa asilimia 58.55 ya kura, kwa sasa yuko La Lanterne, katika makaazi yake huko Versailles, tangu Jumapili jioni. Hapa ndipo mkuu wa nchi anajiandaa kupanda safari yake ya miaka mitano ijayo.

Emmanuel Macron ana wakati wa kuboresha timu yake mpya na kujiandaa kwa siku zijazo. Muda wake unaisha rasmi ndani ya takriban wiki tatu, Mei 13. Sherehe za kutawazwa kwake kama rais zitafanyika kabla ya tarehe hiyo.
Emmanuel Macron ana wakati wa kuboresha timu yake mpya na kujiandaa kwa siku zijazo. Muda wake unaisha rasmi ndani ya takriban wiki tatu, Mei 13. Sherehe za kutawazwa kwake kama rais zitafanyika kabla ya tarehe hiyo. REUTERS - BENOIT TESSIER
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya kwanza inaanza Jumatano Aprili 27 pamoja na kutangazwa rasmi kwa matokeo ya uchaguzi wa urais. Siku hiyo, Emmanuel Macron ataongoza zoezi la kutoa heshima kwa mchekeshaji Michel Bouquet katika makaburi ya mashujaa.

Siku hiyo hiyo, ataongoza Baraza la Mawaziri. Je, kikao hiki kitakuwa cha mwisho na Jean Castex kama Waziri Mkuu? Jean Castex alisema atajiuzulu siku chache baada ya kuchaguliwa tena kwa mkuu wa nchi, lakini kusalia kwake Matignon kwa muda pia kunawezekana.

Emmanuel Macron ana wakati wa kuboresha timu yake mpya na kujiandaa kwa siku zijazo. Muda wake unaisha rasmi ndani ya takriban wiki tatu, Mei 13. Sherehe za kutawazwa kwake kama rais zitafanyika kabla ya tarehe hiyo.

Ziara ya kwanza kama mkuu wa nchi

Baada ya kutawazwa tena, rais anatarajia kufanya ziara kadhaa, hasa katika hospitali ya kijeshi ili kuzungumza na wanajeshi waliojeruhiwa au hata kwenye kaburi ambalo bibi yake amezikwa huko Hautes-Pyrénées.

Na kisha, kwa safari yake ya kwanza nje ya nchi, Emmanuel Macron anapanga kwenda Berlin, Ujerumani, kumtembelea Kansela Olaf Scholz na hivyo kuashiria umuhimu wa ushirikiano wa nchi hizi mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.