Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Zoezi la kuhamisha raia Mariupol "lashindwa" kwa sasa

Katika siku ya 37 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Ijumaa hii, mamlaka za mji wa Mariupol, nchini Ukraine, imesema haiwezekani kwa sasa kuingia katika mji huo na ni hatari kwa watu waliokwama kujaribu kutoka peke yao.

Wakazi karibu na jengo lililoporomoka Machi 30, 2022 huko Mariupol.
Wakazi karibu na jengo lililoporomoka Machi 30, 2022 huko Mariupol. © ALEXANDER ERMOCHENKO/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) inasema imelazimika kusitisha zoezi lake baada ya hali kuona kuwa "haitowezekana kuendelea na zoezi" la uhamishaji kutoka Mariupol. Timu za ICRC zitajaribu tena Jumamosi "kuwezesha kupita kwa usalama kwa raia kutoka Mariupol", mji unaozingirwa na kushambuliwa kwa makombora tangu mwisho wa mwezi Februari na vikosi vya Urusi na ambapo raia 160,000 bado wanaaminika wamekwama katika mji huo.

Akitumia mtandao wa Telegram, mshauri wa meya wa jiji hilo,Petro Andryuschenko, amesema hawaoni nia ya dhati ya Urusi kutoa fursa kwa wakaazi wa mji huo wa Mariupol kuhama hadi katika maeneo ambayo yapo chini ya udhibiti wa Ukraine.

Aliongeza kwamba wavamizi hao, hawakuruhusu kuingia kwa shehena yoyote ya misaada ya kiutu katika mji huo.

Wakati huo huo Urusi inaishutumu Ukraine kwa kutekeleza shambulizi la anga katika ardhi yake Ijumaa hii. Helikopta mbili za Ukraine zimeripotiwa kufanya mashambulizi kwenye kituo cha kuhifadhi mafuta magharibi mwa Urusi, kilomita 40 kutoka mpaka wa nchi hizo mbili.

Angalau maeneo 53 ya kitamaduni yameharibiwa nchini Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi uliozinduliwa Februari 24, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni, UNESCO. Msemaji wa UNESCO amebainisha kuwa orodha hii "si kamilifu".

Kwa upande mwengine mazungumzo ya kati ya Ukraine na Urusi yameanza tena Ijumaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.