Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Zelensky yuko tayari kujadili Donbass na Crimea na Putin

Katika siku ya 27 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumanne Machi 22, fuata taarifa za hivi punde zinazopatikana moja kwa moja.

Uharibifu unaoendelea kusababishwa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, hapa ni moja ya nyumba jijini Kyiv, Machi 21, 2022.
Uharibifu unaoendelea kusababishwa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, hapa ni moja ya nyumba jijini Kyiv, Machi 21, 2022. AP - Vadim Ghirda
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Wanajeshi wa Urusi bado wanajaribu kuizingira kyiv ambapo shambulio la bomu liliua takriban watu wanane usiku wa Jumapili hadi kuamkia Jumatatu.

► Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa Ukraine haitakubali uamuzi wowote kutoka kwa Urusi na kwamba maelewano yoyote yatabidi kwanza yakubaliwe na Waukraine kupitia kura ya maoni.

► Baada ya mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Umoja wa Ulaya, mkuu wa sera ya Mmbo ya Nje wa Umoja wa Ulaya ametangaza kuhusu mkakati wa ulinzi wa umoja huo. Hasa, ameelezea matakwa ya wanachama Ishirini na Saba wa Umoja wa Ulaya wa kuunda kikosi cha haraka cha kupeleka askari 5,000 au kuongeza sehemu ya matumizi ya kijeshi hadi 2% ya Pato la Taifa. Vikwazo vipya dhidi ya Urusi pia vimetangazwa.

► Kulingana na msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi, jeshi la Urusi liko katikati mwa jiji la Mariupol ambapo lilipendekeza kwa mamlaka ya Ukraine kuweka chini silaha zao, bila mafanikio. Ukraine "haitaweka chini silaha zake na kuondoka katika mji uliozingirwa", Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine aliviambia vyombo vya habari vya Ukraine, akijibu makataa yaliyotolewa na Urusi.

► Urusi inadai kuwa imetumia makombora ya hypersonic tangu Ijumaa. Makombora haya yanaweza kuruka kwa karibu kilomita 12,000 kwa saa.

Wakati huo huo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewataja wanajeshi wa Urusi kama "watalii wenye silaha" na "watumwa wa propaganda" ambazo zimebadilisha ufahamu wao. Kiongozi huyo wa Ukraine amesema nchi yake itaangamizwa kabla ya kusalimisha miji yake kwa wanajeshi wa Urusi. Amesisitiza mazungumzo ya moja kwa moja na Rais wa Urusi Vladimir Putin kama hatua muhimu ya kumaliza vita hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.