Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Duru ya tatu ya mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine yaanza

Katika siku ya kumi na mbili ya uvamizi wa Urusi dhii ya Ukraine mnamo Jumatatu (Machi 7), Moscow iliazimia Jumatatu kusitisha mapigano ili kuruhusu kuanzishwa kwa maeneo salama ili kuruhusu raia kuhamishwa kutoka katika miji iliyoshambuliwa kwa mabomu hadi nchini Belarus na Urusi. Duru ya tatu ya mazungumzo ya Urusi na Ukraine  imeanza, nchini Belarus.

Maafisa wa Ukraine na Urusi wanashiriki katika duru ya tatu ya mazungumzo katika eneo la Brest, nchini Belarus mnamo Machi 7, 2022.
Maafisa wa Ukraine na Urusi wanashiriki katika duru ya tatu ya mazungumzo katika eneo la Brest, nchini Belarus mnamo Machi 7, 2022. via REUTERS - BELTA
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Ukraine imeona chaguo "lisilokubalika" la maeneo salama yanayoelekeza raia kwenda Urusi na Belarus. Jeshi la Urusi siku ya Jumatatu lilitangaza kusitisha mapigano ili kuwahamisha raia kutoka miji ya Ukraine ya Kharkhiv, Kyiv, Mariupol na Sumy.

► Kikao cha tatu cha mazungumzo ya kati ya Urusi na Ukraine kimeanza Belarusi Jumatatu hii saa tisa zaa za kimataifa.

► Ulaya inatarajia kuwapokea wakimbizi milioni 5 kutoka Ukraine, kulingana na mkuu wa Sera ya Mambo ya Nje ya Ulaya, Josep Borrell.

► Umoja wa Ulaya unazindua uchunguzi wa wagombea wa Ukraine, Georgia na Moldova.

Mji wa Ufaransa wa Senlis washikamana kuwapokea wakimbizi wa Ukraine

Senlis, mji wenye wakazi zaidi ya 14,000 ulioko takriban kilomita arobaini kutoka mji wa Paris, umeunganishwa na miji ya Kiev-Pechersk nchini Ukraine. Baada ya kutuma michango, jiji hilo linajitayarisha kuwapokea wakimbizi wa kwanza katika familia. Ripoti ya mwanahabari wetu Sylvie Koffi.

IAEA yatoa wito wa "kutopoteza muda" kwa hatari ya ajali ya nyuklia nchini Ukraine

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), ambaye amejitolea kuzuru Ukraine ili kuanzisha mfumo wa kuhakikisha usalama wa maeneo ya nyuklia wakati wa mzozo unaoendelea, amesema anatarajia jibu hivi karibuni. Ametoa wito wa "kutopoteza wakati". "Wakati huu, ikiwa kuna ajali ya nyuklia, sababu haitakuwa tsunami iliyoletwa na asili mama," Rafael Grossi amesema wakati wa mkutano wa Bodi ya maafisa wa IAEA huko Vienna. Badala yake, itakuwa ni matokeo ya kushindwa kwa binadamu kuchukua hatua wakati tulijua tunaweza na tulijua kwamba tulipaswa kufanya hivyo.”

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.