Pata taarifa kuu
UKRAINE-HAKI

ICC yafungua uchunguzi kuhusu hali nchini Ukraine tangu Novemba 2013

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) inafungua uchunguzi kuhusu uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita uliofanywa nchini Ukraine tangu Novemba 21, 2013. Mataifa 39 yamemtaka Mwendesha mashitaka mkuu, kuharakisha kesi hiyo.

Makao makuu ya ICC huko Hague nchini Uholanzi.
Makao makuu ya ICC huko Hague nchini Uholanzi. Wikimédia
Matangazo ya kibiashara

"Kazi yetu ya kukusanya ushahidi inaweza kuanza," alisema Mwanasheria Mkuu, Briton Karim Khan, katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Jumatano jioni Machi 2. Mataifa 39 yalijibu wito wake, aliyotoa mapema wiki hii. Hii ni mara ya kwanza kwa Mahakama! Ombi hili linamruhusu mwendesha mashitaka kuharakisha utaratibu, bila kuomba idhni ya majaji katika hatua hii.

Rasilimali za ziada

Miongoni mwa Mataifa hayo ni yale ya Umoja wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Georgia, Uingereza, Canada na Australia na yale ya Amerika ya Kusini, Costa Rica na Colombia. Karim Khan sasa anaomba ushirikiano wao; ni lazima, lakini juu ya yote unahitaji rasilimali za ziada ili kuweza kufanya utafiti huu. Ushirikiano huo utashughulikia uhalifu wote uliofanywa na pande hizo mbili kwenye mzozo tangu maandamano ya kwanza ya Maidan huko Kiev mnamo msimu wa baridi 2013.

Miaka miwili baadaye, mamlaka mpya ya Ukraine ilimuona mwendesha mashtaka, na kumpa mamlaka ya kisheria juu ya kesi hii. Hata hivyo, Kiev haikujiunga na mkataba wa Mahakama, wala Urusi haikujiunga. Moscow ilipinga kuweka saini yake kwa mkataba ya kuanzisha mahakama hiyo ya kimataifa, lakini haikuwahi kuidhinisha. Kwa hiyo Urusi haina wajibu wa kushirikiana.

Bw Khan, ambaye aliteuliwa kuwa mwendesha mashtaka hivi majuzi, amehakikisha kwamba uchunguzi wake utafanywa "kwa njia yenye malengo na huru" na kwamba utalenga "kuhakikisha uwajibikaji kwa uhalifu ndani ya mamlaka ya ICC". ICC, yenye makao yake makuu mjini The Hague, ilianzishwa mwaka 2002, imewekwa kama mahakama huru ya kimataifa kuwahukumu watu wanaotuhumiwa kwa mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.