Pata taarifa kuu

Le Maire aweka shinikizo kwa kampuni za Ufaransa zinazohusika nchini Urusi

Nchini Ufaransa, Bruno Le Maire ametoa onyo kwa kampuni kadhaa zilizo na shughuli nchini Urusi. Na hasa zile zinzofanya kazi katika sekta ya nishati. Kmpuni kubwa ya Uingereza BP na ile ya  Shell zimeondoka nchini Urusi.

Waziri wa Uchumi wa Ufaransa, Bruno Le Maire, Agosti 30, 2021.
Waziri wa Uchumi wa Ufaransa, Bruno Le Maire, Agosti 30, 2021. REUTERS - SARAH MEYSSONNIER
Matangazo ya kibiashara

"Tutasababisha kuporomoka kwa uchumi wa Urusi", amesema Waziri wa Uchumi wa Ufaransa alipoulizwa kwenye kituo cha france Info, Jumanne hii, Machi 1, juu ya uvamizi unaoendelea wa Urusi dhidi ya Ukraine. "Uwiano wa nguvu za kiuchumi na kifedha uko kabisa kwa Umoja wa Ulaya ambao uko katika mchakato wa kugundua nguvu zake za kiuchumi", ameongeza.

Bruno Le Maire atajadili katika siku zijazo na wakuu kampuni za Engie na TotalEnergies. Lakini Waziri wa Uchumi tayari ameelezea wazi maoni yake, asubuhi ya leo kwenye kituo cha France Info amesema: "Ninaamini kwamba sasa kuna tatizo la kanuni, kufanya kazi na mtu yeyote wa kisiasa au kiuchumi, aliye karibu na utawala wa Urusi. Kwa mara nyingine tena, ni uhuru wa Ulaya ambao unashambuliwa, ni taifa huru ambalo linashambuliwa na kutishiwa na Vladimir Putin”.

TotalEnergies inakataa ufadhili wa miradi mipya nchini Urusi

Kwa niaba ya Engie, hali ni tofauti kidogo kulingana na Bruno Le Maire, kwa sababu msambazaji wa gesi tayari amebadilisha hisa zake katika mradi wa bomba la Nord Stream 2 kuwa mkopo. "Napendelea kuijadili hali hii na mtu wa kwanza anayehusika,ambaye ni Patrick Pouyanné, anayefahamu kabisa uzito wa hali hiyo, anafahamu vyema uzito wa hali hiyo na nadhani tutakuwa uwezo wa kufanya maamuzi pamoja, katika siku zijazo ".

Katika mchakato huo, TotalEnergies imeacha kufadhili miradi mipya nchini Urusi bila kujiondoa kwenye miradi ya sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.