Pata taarifa kuu

Mazungumzo yaanza kati ya Urusi na Ukraine kwa leng la kusitisha vita

Mazungumzo kati ya wajumbe wa Ukraine na Urusi, yanafanyika katika mpaka wa nchi ya Ukraine na Belarus. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, ambayo imevamiwa na Urusi tangu wiki iliyopita, amesema saa 24 zijazo utaamua mustakabali wa nchi yake. 

Wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Februari 28, 2022 huko New York, washirika wa mkutano huo wamesalia kimya kwa dakika moja.
Wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Februari 28, 2022 huko New York, washirika wa mkutano huo wamesalia kimya kwa dakika moja. © AP/John Minchillo
Matangazo ya kibiashara

Wakati mazungumzo hayo yakiendelea, kwa siku ya tano, mapigano yameendelea kati ya mataifa hayo jirani, huku kukiwa na ripoti ya kutokea kwa mauaji ya raia katika mji wa Kharkiv. 

Wizara ya afya nchini Ukraine, imesema, vita hivyo vimesababisha vifo vya watu zaidi ya 350 wakiwemo watoto 14, huku jeshi la Ukraine likisema, mashambulizi ya Urusi yamepungua. 

Hata hivyo, Ukraine inasema bado vikosi vya Urusi vinalenga kuteka mji mkuu Kyiv , wakati huu mapigano yakishuhudiwa katika bandari ya Odessa na karibu na mji wa Ochakiv. 

Urusi nayo inaendelea kudai kuwa, imetawala angaa la Ukraine baada ya kurusha makombora 30 na kutekeleza mashambulizi ya anga manne siku ya Jumapili. 

Ukraine nayo imedai imewauwa wanajeshi 4300 wa Urusi na kufanikiwa kuzuia mashambulizi kadhaa kufika katika jiji la Kiev. 

Katika hatua nyingine, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema imeweka tayari kikosi chake cha kurusha mizinga nchini Ukraine baada ya agizo la rais Putin. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.