Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Watu 50,000 wakimbilia nje ya nchi kulingana na Umoja wa Mataifa

Vita vinaendelea nchini Ukraine na kulingana na vyanzo kadhaa wanajeshi wa Urusi wameukaribia kabisa mji mkuu wa Ukraine, Kiev. Huu ni uvamizi wa Urusi katika nchi yenye kuzingatia mifumo ya kidemokrasia na ambao umeongeza hofu ya kutokea vita vipana katika bara la Ulaya na kuchochea pia juhudi za ulimwengu za kutaka kuizuia Urusi.

Raia wa Ukraine wakiondoka kwenye treni iliyobeba watu 275, wakiwasili Zahony, nchini Hungary, mji wa mpakani na Ukraine, Ijumaa, Februari 25, 2022.
Raia wa Ukraine wakiondoka kwenye treni iliyobeba watu 275, wakiwasili Zahony, nchini Hungary, mji wa mpakani na Ukraine, Ijumaa, Februari 25, 2022. AP - Anna Szilagyi
Matangazo ya kibiashara

Urusi inadai imeshauteka uwanja wa ndege muhimu unaoiunganisha Kiev na nchi za Magharibi na itautumia kusafirisha haraka wanajeshi wake kuingia kwenye mji huo.

Jeshi la Urusi limesema limeshaudhibiti uwanja muhimu wa ndege wa kimkakati ulioko nje ya Kiev ambao unaiwezesha nchi hiyo kupeleka haraka wanajeshi wake katika mji mkuu, Kiev.

Kadhalika Urusi imedai kwamba tayari imeshautenganisha mji huo na nchi za Magharibi kwa maana ya kuyadhibiti maeneo mengi ambayo ni njia wanayoelekea watu wengi wanaokimbia uvamizi, huku misururu ya magari ikionekana ikielekea eneo la mpakani na Poland.

Maafisa wa Ukraine wametumia magari ya kijeshi pamoja na magari ya kuzowa theluji kuulinda mji wa Kiev na kuzuia watu kutembea. Lakini pia maafisa wa Ukraine wamesema majasusi wa Urusi wanahangaika kutafuta namna ya kuingia katika mji huo.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema wanaandaa hatua za kuwezesha mamilioni ya wananchi kuondoka Ukraine. Pia Umoja wa Mtaifa umetangaza kwamba watu 50,000 tayari wameikimbilia katika nchi jirani.

Marekani na nchi nyingine zenye nguvu duniani wameiwekea vikwazo vikali kabisa Urusi na uvamizi wa Urusi unaweza kuiongezea hata zaidi nchi hiyo vikwazo vya kiuchumi na usambazaji wa nishati, na kutishia kutokea hali mbaya zaidi ya kuwaumiza wananchi wa kawaida wa Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.