Pata taarifa kuu

Vladimir Putin : Niko hapa kwa kutetea maslahi ya nchi

Siku moja baada ya kutangaza kutambua uhuru wa maeneo yaliyojitenga ya Donetsk na Lugansk, rais wa Urusi ametangaza tishio la vita vikubwa. Jumatano hii, Februari 23, Vladimir Putin pia amesisitiza juu ya hali "isiyojadiliwa" ya maslahi na usalama wa nchi yake, huku akisema hata hivyo yuko tayari kupata "suluhu za kidiplomasia".

Jumatano hii, Februari 23, Vladimir Putin (kwenye picha) amesisitiza juu ya hali ya "kutojadiliwa" ya maslahi na usalama wa nchi yake, huku akisema hata hivyo yuko tayari kupata "suluhu za kidiplomasia".
Jumatano hii, Februari 23, Vladimir Putin (kwenye picha) amesisitiza juu ya hali ya "kutojadiliwa" ya maslahi na usalama wa nchi yake, huku akisema hata hivyo yuko tayari kupata "suluhu za kidiplomasia". AP - Sergey Guneev
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuomba jeshi lake "kulinda amani" katika maeneo ya yaliyojitenga ya Donetsk na Lugansk, ambayo alitambua uhuru wake, Vladimir Putin alipata idhni kutoka kwa Baraza la Wawakilishi kupeleka majeshi katika maeneo yaliyo jitenga ya Ukraine. NATO sasa inasema inatarajia "shambulio kubwa".

Lakini kufuatia agizo la Bw Putin la kutuma wanajeshi katika mikoa ya Ukraine inayoshikiliwa na waasi ya Donetsk na Luhansk, Ujerumani ilitangaza kuwa inasitisha mchakato wa kutoa leseni ya bomba kati yake na Urusi na uendeshaji - na hivyo kusimamisha mradi huo .

Hatua hiyo ni kubwa kwani Urusi inaipatia Ulaya karibu 40% ya gesi yake, inayopatikana kutoka kwa usambazaji mkubwa mashariki mwa Urusi.

Umoja wa Ulaya umeahidi kuchukuwa vikwazo kuwalenga wabunge wa Urusi, benki zinazofadhili jeshi la Urusi pamoja na uwezo wa serikali ya Urusi kufikia masoko ya fedha ya jumuiya hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.