Pata taarifa kuu

Uchaguzi wa urais: Tangazo la kuondoka kwa jeshi nchini Mali lazua taharuki

Baada ya tangazo la Emmanuel Macron na washirika wake la kujiondoa kijeshi nchini Mali, kulikuwa na hisia nyingi, hasa nchini Ufaransa, miezi miwili kabla ya uchaguzi wa urais.

Wanajeshi wa Ufaransa kwenye kambi ya MJINI Gao, Mali, mnamo mwaka wa 2012.
Wanajeshi wa Ufaransa kwenye kambi ya MJINI Gao, Mali, mnamo mwaka wa 2012. AP
Matangazo ya kibiashara

Chini ya miezi miwili kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa, tangazo la jeshi la Mali kujiondoa katika Operesheni Barkhane limeibua hisia kali kutoka kwa chama cha walio wengi, na vile vile kambi ya upinzani.

"Dhamira yetu katika ukanda wa Sahel ya kupambana dhidi ya wanajihadi haijaisha," amesema mgombea urais wa chama cha LR, Valérie Pécresse, kwenye kituo cha habari cha LCI. Amebainisha kwamba alitaka, kama alivyo tangaza rais w

Naye katibu wa kwanza wa chama amesifu "operesheni muhimu sana". Wafaransa lazima wabaki "katika hali nyingine" katika ukanda wa Sahel, kulingana na Olivier Faure.

Kwa upande wake, mgombea wa Chama cha Kikomunisti amebaini kwamba Ufaransa "lazima ijitoe" lakini "lazima zaidi ya yote ibadilishe sera". "Suluhisho halitakuwa la kijeshi, litakuwa la ushirikiano na maendeleo", amesema Fabien Roussel kwenye kituo cha Cnews, kabla ya kukumbusha upinzani wake na kukosoa vikwazo vilivyowekwa na ECOWAS kufuatia mapinduzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.