Pata taarifa kuu
UINGEREZA-HAKI

WikiLeaks: Julian Assange ana hatari ya kujiua iwapo atakabidhiwa Marekani

Majaji wa Mahakama Kuu ya London wametoa wito wa kusema iwapo wataunga mkono au kubatilisha kukataa kumsafirisha raia wa Australia mwenye umri wa miaka 50, ambaye anakabiliwa na kifungo cha miaka 175 nchini Marekani.

Julian Assange anakabiliwa na kifungo cha miaka 175 nchini Marekani.
Julian Assange anakabiliwa na kifungo cha miaka 175 nchini Marekani. Pedro Pardo AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Licha ya kuhakikishiwa na Washington juu ya hatima ya mwanzilishi wa WikiLeaks, mawakili wake wamesisitiza siku ya Alhamisi juu ya hatari ya kujiua kwa Julian Assange iwapo atakabidhiwa Marekani.

Majaji wa Mahakama Kuu ya London watatakiwa kusema kama wanaunga mkono au kubatilisha kukataa kumsafirisha raia wa Australia mwenye umri wa miaka 50, ambaye anakabiliwa na kifungo cha miaka 175 jela kwa kufichua mamia kwa maelfu ya nyaraka zilizoainishwa.

Uamuzi wao hautarajiwi kwa wiki kadhaa.

Ikiwa Marekani itafaulu, uamuzi wa Januari utabatilishwa na mahakama ya Uingereza italazimika tena kuamua. Na kwa yeyete atakayeshindwa, ana fursa ya kuwasilisha malalamiko yake katika Mahakama ya Juu ya Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.