Pata taarifa kuu
INDIA

INDIA: 6 wathibitishwa kuambukizwa aina mpya ya virusi vya Covid 19 kutokea Uingereza

Mamlaka za afya nchini India, zimeripoti watu 6 kuambukizwa aina mpya ya virusi vya Covid 19 ambavyo chimbuko lake ni nchini Uingereza, maambukizi ambayo yamesababisha mataifa kadhaa ulimwenguni kufunga mipaka yake na Uingereza.

Wafanyakazi wa afya nchini India, wakiwa wamevalia mavazi maalumu ya kujikinga na Covid 19
Wafanyakazi wa afya nchini India, wakiwa wamevalia mavazi maalumu ya kujikinga na Covid 19 REUTERS/P. Ravikumar/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya afya inasema abiria wote 6 waliwasili wakitokea nchini Uingereza na kwamba tayari wametengwa, huku watu wao wa karibu waliokutana nao nao wakitengwa.

Ikiwa na maambukizi ya watu karibu milioni 10, nchi ya India ni taifa la pili dunini kuathirika zaidi na virusi vya corona baada ya Marekani.

Karibu watu laki 1 na elfu 50 wameshafariki nchini India kutokana na virusi hivyo, huku siku ya Jumanne ikirekodi maambukizi mapya elfu 16.

Taifa la India, limesitisha safari zote za ndege na nchi ya Uingereza hadi mwishoni mwa mwezi, lakini abiria zaidi ya elfu 33 walisafiri kutoka Uingereza na kuingia nchin humo mwezi Novemba peke yake, kabla ya makataa haya kuanza kutekelezwa.

Miongoni mwa waliowasili, watu 114 walithibitishwa kuwa na maambukizi ya Covid 19 na sampuli zao zinafanyiwa uchunguzi zaidi ikiwa wameambukizwa aina mpya ya virusi vya corona, ambavyo vimeripotiwa kwenye mataifa ya Ulaya na Asia.

Mamlaka nchini humo zinajiandaa kutoa chanjo kwa zaidi ya watu milioni 300 kuanzia mwezi ujao, ambapo taifa hilo linauwezekano wa kuthibitisha chanjo ya AstraZeneca na ile ya chuo kikuu cha Oxford, baada ya kuawasilisha nyaraka zaidi kuthibitisha ufanisi wake.

Chanjo ya The AstraZeneca-Oxford, inaelezwa kuwa ya bei rahisi ukilinganisha na chanjo zingine na pia ni rahisi katika usafirishaji wake na inahitaji jokofu la kawaida kuhifadhi kwenye ubaridi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.