Uingereza yawa taifa la kwanza kuidhinisha chanjo ya Pfizer
Uingereza imekuwa nchi ya kwanza duniani kuidhinisha matumizi ya chanjo dhidi ya COVID-19 iliyotengenezwa na maabara ya Marekani ya Pfizer na mshirika wake BioNTech kutoka Ujerumani.
Imechapishwa:
"Chanjo hii itapatikana nchi nzima kuanzia wiki ijayo," serikali ya Uingereza imesema leo Jumatano katika taarifa.
Matumizi haya yameidhinishwa na mamlaka ya dawa nchini Uingereza, Medicines and Healthcare Products Regulatory Agency (MHRA), mamlaka ya afya ya kwanza duniani kuchukua uamuzi kama huo.
Hakuna chanjo yoyote ambayo imeidhinishwa katika nchi yoyote duniani.
"Hii ni habari njema sana," amesema Waziri wa Afya wa Uingereza Matt Hancock.
Katika taarifa, maabara ya Marekani ya Pfizer yamebaini kwamba dozi za kwanza zitaweza kutolewa "mara moja" na kusema kuwa idhini hii ya kwanza ni "mafanikio" katika vita dhidi ya janga COVID-19.