Pata taarifa kuu
HISPANIA-CORONA

Coronavirus: Visa vipya 20,000 vyathibitishwa Uhispania tangu Ijumaa

Uhispania imeendelea kurekodi idadi kubwa ya visa vipya vya maambukizi ya virusi vya Corona tangu Ijumaa ya wiki iliyopita.

Nchi ya Hispania ni miongoni mwa mataifa yenye idadi ya juu ya maambukizi.
Nchi ya Hispania ni miongoni mwa mataifa yenye idadi ya juu ya maambukizi. © Jose Jordan / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu wiki hii Uhispania imerekodi visa vipya zaidi ya 19,979, sawa na idadi ya wastani wa visa vipya 6,659 kwa siku, kwa jumla ya visa 1,648,187 vilivyothibitishwa tangu kuzuka kwa janga hilo nchini humo.

Wizara ya afya ya Uhispania pia imeripoti vifo vipya 943 vinavyohusiana na janga la Covid-19 katika kipindi cha siku saba zilizopita, sawa na idadi ya wastani 134 kwa kila siku, dhidi ya 1,177 siku ya Ijumaa.

Tangu kuzuka kwa janga hilo, ugonjwa huo wa Covid-19 umeua watu 45,069 nchini Uhispania.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.