Pata taarifa kuu
VATICAN

Vatican: Wilton Gregory kutawazwa kuwa kadinali wa kwanza mweusi kutoka Marekani

Jumamosi hii, Novemba 28, Wilton Gregory atakuwa kiongozi wa kwanza mweusi kutoka Marekani kutawazwa na kiongozi wa Kanisa Katoliki kuwa kardinali, pamoja na viongozi wengine kumi na wawili.

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis.
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis. AP Photo/Gregorio Borgia
Matangazo ya kibiashara

Wilton Gregory pia alikuwa askofu mkuu wa kwanza mweusi huko Washington.

 

Kwa siku kumi, amewekwa karantini katika jengo la kifahari huko Vatican. Wilton Gregory amekuwa akifanya mahojiano tu kwa dakika chahe kwa njia ya mtandao na chakula chake kimekuwa kikipitishwa chini ya mlango ya chumba anakolala kwa kusubiri siku hii ya kipekee ya leo.

 

Tahadhari muhimu kabla ya sherehe ya Jumamosi hii wakati ambapo Askofu Mkuu wa Washington atapiga magoti mbele ya Papa kupokea kofia yake yenye pembe nne na ya rangi ya zambarau, na kuwa kadinali wa kwanza mweusi kutoka Marekani.

 

Kwa miezi kumi na nane, Wilton Gregory, 72, alikuwa tayari askofu mkuu wa kwanza mweusi wa Washington.

 

Wilton Gregory ni mmoja wa viongozi wa kidini nchini Marekani ambaye alimtia hatiani na kumkosoa rais Donald Trump kwa matamshi yake siku moja baada ya vikosi vya usalama vya Marekani kuzima kwa nguvu kupita kiasi maamndamano ya kupinga ubaguzi wa rangi.

 

Wilton Gregory amekuwa akilaani vitendo vya unyanyasaji wa kingono vilivyodaiwa kutekelezwa na baadhi ya makasisi wa kanisa Katoliki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.