Pata taarifa kuu
UINGEREZA- CORONA

Coronavirus: London yaomba MHRA kutathmini chanjo iliyotengenezwa na AstraZeneca

Uingereza imelitaka shirika linalodhibiti Dawa na Bidhaa za Afya nchini Uingereza (MHRA) kutathmini chanjo dhidi ya COVID-19 iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford na kampuni ya AstraZeneca kwa ajili ya biashara.

Ugonjwa hatari wa COVID-19 umeua watu wengi duniani.
Ugonjwa hatari wa COVID-19 umeua watu wengi duniani. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kampuni ya AstraZeneca inatarajia dozi milioni 4 zitapatikana nchini Uingereza mwishoni mwa mwezi ujao, na Waziri wa Afya wa Uingereza Matt Hancock anatarajia chanjo hiyo itapatikana kabla ya Krismasi.

 

"Tumeomba rasmi shirika linalodhibiti Dawa na Bidhaa za Afya (MHRA) kutathmini chanjo ya kampuni ya AstraZeneca, kuthibitisha takwimu na kubaini ikiwa inakidhi viwango vya usalama," Matt Hancock amesema katika taarifa.

 

"Barua hii ni hatua muhimu kuelekea kutumwa kwa chanjo haraka na salama iwezekanavyo., " waziri wa afya wa uingereza ameongeza.

 

Shirika la kudhibiti Dawa na Bidhaa za Afya nchini Uingereza tayari linatathmini chanjo ili takwimu juu ya usalama na ufanisi wake vichapishwe.

 

Jumatatu wiki hii kampuni ya AstraZeneca ilitangaza dawa yake ya chanjo dhidi ya COVID-19, iliyetengenezwa kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Oxford, ina nguvu za kutibu COVID-19 kwa 90% kulingana na matokeo ya awali kutoka jaribio la kliniki la awamu ya tatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.