Pata taarifa kuu
SWEDEN-CORONA-AFYA

COVID-19: Watu 6,000 wafariki dunia nchini Sweden, Waziri Mkuu Stefan Löfven karantini

Nchini Sweden, Waziri Mkuu Stefan Löfven ametangaza kwamba ameamua kujiweka kizuizini baada ya kutangamana na mtu aliyeambukizwa virusi vya Corona.

Waziri Mkuu wa Swiden Stefan Löfven katika mkutano na waandishi wa habari juu ya janga la COVID-19 nchini Sweden, huko Stockholm.
Waziri Mkuu wa Swiden Stefan Löfven katika mkutano na waandishi wa habari juu ya janga la COVID-19 nchini Sweden, huko Stockholm. TT News Agency/Pontus Lundahl via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Visa vya maambukizi vinaendelea kuongezeka nchini Sweden, kama sehemu zingine Ulaya, na idadi ya vifo tangu kuzuka kwa janga hilo imezidi 6,000.

Hata hivyo mamlaka bado inakataa kuagiza wartu kuvaa barakoa, au kupiga marufuku watu kutembea.

Wimbi la pili la mlipuko wa virusi vya Corona, ambalo lilikuwa limechelewa kuingia Sweden, sasa linaonekana kuathiri baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.

Siku ya Alhamisi, Novemba 5, watu 90 walifanyiwa matibabu katika uangalizi mkubwa, dhidi ya 56 wiki mbili zilizopita. Idadi ya vifo vya kila siku, ambayo ilikuwa ya watu wawili hadi watatu, sasa inapita kati ya watu watano na saba.

Waziri Mkuu Stefan Löfven, ambaye amejiweka karantini baada ya kukaribiana an mtu aliyeambukizwa virusi vya Corona, amesema nchi yake inakumbwa na hali ni mbaya sana. Katika mikoa mingi, kizingiti cha mikutano ya hadhara kimepunguzwa hadi watu 50, na hatua kadhaa zimechukuliwa: Wasweden wamependekezwa kupunguza mawasiliano yao ya kijamii na kuepuka maeneo yaliyofungwa.

Ni kupendekezwa, wala sio kulazimishwa, hiyo ndiyo kanuni ya mapendekezo. mamlaka wanaesema kiwango cha vifo bado hakijafika katika kiwango cha nchi zilizoathirika zaidi za Ulaya, kama Ufaransa, ambayo kwenye kiashiria hiki inaongoza dhidi ya Sweden, mamlaka ya Sweden imesema katika taarifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.