Pata taarifa kuu
UFARANSA-MALI-USALAMA

Mateka wa zamani wa Ufaransa Sophie Pétronin awasili Paris

Ndege iliyokuwa imembeba mateka wa zamani wa Ufaransa Sophie Pétronin imetua kwenye uwanja wa ndege wa Villacoublay karibu na mji wa Paris.

Sophie Pétronin akiwasili nchini Ufaransa, Oktoba 9, 2020.
Sophie Pétronin akiwasili nchini Ufaransa, Oktoba 9, 2020. RFI/Valérie Gas
Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo ilikuwa ilinyanyuka mapema saa chache kutoka mji mkuu wa Mali, Bamako. Sophie Pétronin, Mfaransa mwenye asili ya Uswisi amekuwa akizuiliwa na wanamgambo wa Kiislam kwa karibu miaka minne huko Sahel.

Alipowasili kwenye uwanja wa ndege amepokelewa na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Karibu na Sophie Pétronin katika ndege hiyo alikuwepo mtoto wake, Sébastien Chadaud, ambaye aliwasili nchini Mali mapema wiki hii. Kulikuwa pia na madaktari wawili waliohusika na kufuatilia hali ya afya ya mateka huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 75.

Pétronin amekuwa akielezwa kuwa mateka wa mwisho wa Ufaransa kushikiliwa popote duniani.

Sophie Petronin, mfanyakazi wa mashirika ya misaada, raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 75, aliyetekwa mwaka 2016 aliwasili jiini Bamako pamoja na mwanasiasa wa nchini Mali, Soumaila Cisse.

Mateka hao wa zamani baadae walielekea katika Ikulu ya rais ilipo Kuoulouba ambako walikutana na rais wa kipindi cha mpito Bah N'Daw, na baadae Sophie Pétronin aliekea ubalozi wa Ufaransa.

Awali Serikali ya Mali ilitangaza kuachiliwa huru kwa Waitaliano Nicola Chiacchio na Pier Luigi Maccalli. Majina yao yalikuwa hayajawahi kuonekana hadi wakati wanapoachiwa huru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.