Pata taarifa kuu
UFARANSA-USALAMA

Visa vya ubaguzi wa rangi vilishuka kwa kiasi kikubwa mwaka 2017 Ufaransa

Ripoti rasmi kutoka nchini Ufaransa imeeleza kuwa, matukio ya ubaguzi wa rangi yanayo sababisha mashambulizi ya kimwili yamepungua kwa ujumla nchini Ufaransa mwaka jana, licha ya kuongezeka kwa vurugu dhidi ya Wayahudi na Waislamu.

Maandamno dhidi ya ubaguzi wa rangi na uhamiaji nchini Ufaransa, Jumamosi, Mei 28, 2011, huko Paris.
Maandamno dhidi ya ubaguzi wa rangi na uhamiaji nchini Ufaransa, Jumamosi, Mei 28, 2011, huko Paris. AFP/Bertrand Guay
Matangazo ya kibiashara

ufuatia mashambulizi ya kigaidi ya Januari na Novemba mwaka 2015, matukio kadhaa yaliripotiwa Polisi ikiwa ni pamoja na vitendo vya vurugu, moto na uharibifu, pamoja na vitisho kwa watu zaidi ya 2,000.

Matukio ya ubaguzi wa rangi yameshuka kwa kiasi kikubwa mwaka 2016 na mwaka jana, matukio 950 yaliripotiwa ikiwa ni sawa na kupungua kwa asilimia 16%.

Hata hivyo,vitendo ya unyanyasaji dhidi ya waliowachache vineongezeka kutoka 67 hadi 72 dhidi ya Waislamu na 77 hadi 97 dhidi ya Wayahudi, kulingana na ripoti hiyo.

Waziri mkuu wa Ufaransa Eduard Philippe amesema kupiga vita ubaguzi wa rangi ni kutekeleza kwa vitendo.

Tukio la kushambuliwa hivi majuzi kwa mtoto mmoja wa Kiyahudi mwenye umri wa miaka 8 katika eneo la Sarcelles kaskazini mwa jiji la Paris lililaaniwa vikali na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.