Pata taarifa kuu

Hollande, Merkel na Putin wakubaliana kwa mkutano wa kilele kufanyika mjini Berlin

François Hollande alikutana kwa mazungumzo Jumatano hii na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Urusi Vladimir Putin kujadili mkutano wa kilele kuhusu Ukraine ambao unaweza kufanyika "hivi karibuni" mjini Berlin lakini tarehe ya mkutano huo haijatangazwa, Ofisi ya rais wa Ufaransa imesema katika taarifa yake. Tangazo hili linakuja siku moja baada ya mtafaruku wa kidiplomasia kati ya marais wa Ufaransa na Urusi.

Kutoka kushoto kwenda kulia: Vladimir Putin, François Hollande, Petro Poroshenko na Angela Merkel, Februari 11, 2015 katika mji wa Minsk, Belarus.
Kutoka kushoto kwenda kulia: Vladimir Putin, François Hollande, Petro Poroshenko na Angela Merkel, Februari 11, 2015 katika mji wa Minsk, Belarus. AFP PHOTO / MAXIM MALINOVSKY
Matangazo ya kibiashara

Ilikua kwenye mazungumzo kwa njia ya simu ambapo viongozi hawa watatu walifanya 'kazi kwa pamoja ili kujenga mazingira kwa ajili ya mkutano wa kilele' kati ya Ufaransa, Ujerumani, Urusi na Ukraine, 'ambao unaweza kufanyika hivi karibuni mjini Berlin,' Ikulu ya Elysee imesema katika taarifa yake. François Hollande na Angela Merkel watakutana Alhamisi hii na Rais wa Ukraine Petro Poroshenko, Ikulu ya Elysée imeongeza.

"Utatuzi wa mgogoro mashariki mwa Ukraine unatakiwa kuanza kwa usitishwaji wa mapigano, kuharakisha shughuli mbalimbali za kurejesha amani na kuingia bila kuzuiliwa kwaujumbe uchunguzi wa jumuiya ya amani na Usalama wa Ualaya hadi kwenye mpaka", Ikulu ya Elysée imebaini.

Watu 9600 wapoteza maisha tangu Aprili 2014

Mkutano huu utakaozishirikisha nchi nne unatazamiwa kufanyika wakati ambapo kunaripotiwa mvutano wa kidiplomasia kati ya Ufaransa na Urusi kuhusu suala la Syria, mvutano ambao Jumanne wiki hii, ulisababisha Vladimir Putin kufuta ziara yake angeliifanya Oktoba 19 mjini Paris. François Hollande alisema Jumanne kuwa kuna 'maendeleo madogo' katika kutatua mgogoro wa Ukraine, akisema yuko "tayari wakati wowote" katika kuandaa mkutano huu.

Ukraine inakabiliwa kwa zaidi ya miaka miwili na mgogoro kati ya vikosi vyake waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki ambao wanaungwa mkono kijeshi na Urusi, kwa mujibu wa serikali ya Kiev na nchi za Magharibi, tuhuma ambazo serikali ya Moscow inakanusha. Machafuko hayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 9,600 tangu mwezi Aprili 2014, licha ya kuanzishwa kwa mikataba kadhaa ya kusitisha mapigano, mapigano makali yalitokea mara kwa mara katika uwanja wa mapigano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.