Pata taarifa kuu
UFARANSA-HOLLANDE

François Hollande ziarani Ureno

Rais François Hollande ameanza Jumanne hii nchini Ureno ziara ya kikazi barani Ulaya kwa lengo la kuandaa uzinduzi wa Umoja wa Ulaya, chini ya ishara ya usalama na ulinzi baada ya shambulizi jipya nchini Ufaransa.

Rais wa Ufaransa François Hollande
Rais wa Ufaransa François Hollande REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Baada ya maombolezo ya kitaifa ya siku tatu kwa kuwakumbuka wahanga 84 wa mashambulizi kwa kutumia lori mjini Nice, rais wa Ufaransa atazuru Jumanne hii mji wa Lisbon na Alhamisi wiki hii mji wa Dublin kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa kilele muhimu utakaofanyika mwezi Septemba kuhusu mustakabali wa Ulaya.

Hata hivyo aliahirisha hatua kadhaa za ziara yake, hasa katika miji ya Vienna, Prague, Bratislava, ziara iliyokua imepangwa kufanyika wiki hii wakati Ufaransa ikiwa bado katika majonzi ya mashambuliziyaliyodaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State (IS).

Pia amefupiza ziara yake ya mjini Lisbon kwa sababu ya kikao cha Baraza la Mawaziri Jumanne hii asubuhi juu ya kuongezewa muda kwa hali ya tahadhari, ambayo itapelekea kufanyika Bungeni mjadala mkali Jumanne hii jioni.

Hata hivyo François Hollande anakabiliwa na upinzani mkali kutoka vyama vya mrengo wa kulia na ambavyo vinadai kwamba sera zake zaugaidi hazitoshi.

Chama cha Republican kimeweka masharti kadhaa kwa kuweza kupigia kura muda wa kuongezwa kwa hali ya tahadhari na kuomba kuundwa kwa tume ya wabunge itakayofanya uchunguzi kuhusu mazingira ya mashambulizi ya 13 Novemba Paris Paris yaliyosababisha watu 130 kuawa na yale ya Machi 22 mjini Brussels yaliyosababisha vifo vya watu 32.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.