Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-ASSANGE

Julian Assange: "Ulaya itakuwa vizuri bila ya Uingereza"

Mwasisi wa Wikileaks, Julian Assange amesema anaunga mkono Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya, kwa sababu za kisiasa, lakini pia za kibinafsi.

Julian Assange, mwasisi wa Wikileaks.
Julian Assange, mwasisi wa Wikileaks. © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Julian Assange amevunja ukimya wake na kutoa msimamo wake juu ya htama ya Ulaya iwapo Uingereza itajiondoa katika Umoja wa Ulaya. Bw Assange ameyazungumza hayo akiwa katika ubalozi wa Equador nchini Uingereza alikokimbilia.

"Kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya, ninaunga mkono kabisa ! Na si kwa sababu tu ya maslahi yangu binafsi: kama Uingereza inaondoka katika Umoja wa Ulaya, hati ya kukamatwa iliyotolewa dhidi yangu itakua haina kazi tena. Hapana, kama naunga mkono, ni kwa sababu hasa za kisiasa, " amesema katika makala yaliyochapishwa kwenye FRANCETV INFO.

Mpaka sasa, Ulaya haifikii kutekeleza mageuzi ambayo inahitaji, kutokana na Uingereza kuendelea kusalia katika Umoja wa Ulaya.

Na ameaongeza: "kuondoka kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya ni kama kura ya maoni kwa uhuru wa Scotland," amedai.

"Ulaya inahitaji mageuzi. Lakini haiwezi kuyafiki bila kupta mshtuko. Kuondoka kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya, ambapo kunazuia mambo mengi, itakua mshtuko mkubwa ambao utaleta mageuzi halisi, kwa zaidi ya ushirikiano wa kisiasa na kijamii", amesema Assange.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.