Pata taarifa kuu
UGIRIKI-ULAYA-UCHUMI

Ugiriki: Athens yasubiri wakopeshaji wake

"Taasisi", zinazojulikana pia kama Troïka au wakopeshaji, wanatazamiwa kurejea katika mji mkuu wa Ugiriki, Athens leo Ijumaa baada ya kukosekana kwa miezi kadhaa. Kuwasili kwao kutaashiria mwanzo wa mazungumzo kuhusu mpango wa tatu wa msaada.

Baada ya mifumo miwili ya mwanzo ya mageuzi kupitishwa na Bunge la Ugiriki, Athens inasubiri mpango mpya wa msaada.
Baada ya mifumo miwili ya mwanzo ya mageuzi kupitishwa na Bunge la Ugiriki, Athens inasubiri mpango mpya wa msaada. REUTERS/Ronen Zvulun
Matangazo ya kibiashara

Hili ni suala nyeti la kisiasa kwa serikali ya Alexis Tsipras. Baada tu ya uchaguzi wa mwezi Januari, waziri wake wa zamani wa fedha, Yanis Varoufakis, alisema kuwa hawezi tena kushirikiana na taasisi tatu zinazotoa mikopo kwa nchi ya Ugiriki, zinazojulikana kama Troïka. Leo ni vigumu kukana wakati ambapo Waziri mkuu wa Ugiriki anatafuta kwa gharama zote ili akamilishe makubaliano kuhusu mpango wa tatu wa msaada. Hata wakuu wa ujumbe wa wakopeshaji wanarejea katika mji mkuu wa Ugiriki, Athens, baada ya kukosekana kwa mwaka mmoja. Majadiliano yao yalifanyika kwa utulivu zaidi katika mji mkuu wa Ufaransa.

Hata hivyo, busara bado inahitajika. Mpango wa wageni hautotangazwa. Pia ni vigumu kujua sehemu ambapo watakutana na washirika wao kutoka Ugiriki. Hata hivyo, ni serikali ya Ugiriki ambayo imetangaza ujio wa wakopeshaji hao. Wakopeshaji hao, hasa Shirika la fedha duniani (IMF), wamekataa kwa sasa kuthibitisha. Mmoja wa wajumbe katika mazungumzo hayo alithibitisha Alhamisi mchana wiki hii kwamba tiketi ya ndege ilikuwa bado haijanunuliwa.

Mwanzo wa mazungumzo kwa mpango mpya wa msaada

Kuwasili kwa wakopeshaji hawa katika mji mkuu wa Ugiriki, Athens, ni ishara ya mazungumzo kuhusu mpango wa tatu wa msaada. ilikua inabidi kwanza Bunge la Ugiriki litowe idhni kwa mkataba uliofikiwa mjini Brussels Julai 13. Mfumo wa kwanza wa mageuzi ulipitishwa siku mbili zilizopita na mpango wa pili ulipitishwa Alhamisi wiki hii, kwa hiyo wataalam wataweza kuingia katika mazungumzo ya moja kwa moja. Bunge la Ugiriki (Vouli) linatazamiwa kutoa msimamo wake kwa mara nyingine tena kuhusu baadhi ya masuala, kama vile kodi kwa wakulima au pensheni, lakini yote hayo hayatazuia mazungumzo kwenda vizuri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.