Pata taarifa kuu
UFARANSA-UKOMBOZI

Ufaransa: gwaride la Julai 14 kati ya enzi za zamani na sasa

Ufaransa inaadhimisha leo Jumanne Julai 14 miaka sabini tangu kumalizika kwa vita vikuu vya pili vya dunia.

Raid, kitengo rasmi cha polisi ta taifa ya Ufaransa,  wakifanya mazoezi kwa ajili kushiriki kwa mara ya kwanza gwaridembele ya Ikulu ya Champs Elysées. Paris, Machi 12 mwaka 2015.
Raid, kitengo rasmi cha polisi ta taifa ya Ufaransa, wakifanya mazoezi kwa ajili kushiriki kwa mara ya kwanza gwaridembele ya Ikulu ya Champs Elysées. Paris, Machi 12 mwaka 2015. AFP PHOTO / LOIC VENANCE
Matangazo ya kibiashara

Mwaka huu 2015 tarehe hii inatoa heshima kwa vikosi viliyopambana kwa kulikomboa taifa la Ufaransa kutoka mikononi mwa utawala wa kiimla wa Kinazi. Lakini siku hii inafika baada ya miezi sita kutokea kwa mashambulizi katika mji wa Paris. Mwaka 2015 ulikua pia wa mapambano dhidi ya ugaidi.

Gwaride la kijeshi linatazamiwa kufanyika leo, katika hali ya kuadhimisha miaka sabini tangu kutokea kwa vita vikuu vya pili vya dunia.

Tarehe 16 Novemba mwaka 1940, alipotokea uhamishoni mjini London, nchini Uingereza, jenerali de Gaulle alitoa Amri ya kulikomboa taifa la Ufaransa kutoka mikononi mwa utawala wa kiimla wa Kinazi. Jenerali de Gaulle aliendesha vita dhidi ya ukoloni huo hadi kuhakikisha kuwa Ufaransa inakua huru.

Katika Utawala wa Vichy watu ikiwa ni pamoja na wanajeshi pamoja na raia wa kawaida waliojitolea kwa kazi nzuri ya kulikomboa taifa la Ufaransa kufidiwa. Watu 1,038 walijikuta wakipewa tuzo ya Ukombozi. Miongoni mwa watu hao sita pekee ndio bado wako hai. Na wale ambao afya yao bado inawaruhusu watakuwepo katika jukwaa la rais, wakikaa pembezoni mwa rais wa Ufaransa, Francois Hollande.

Lakini gwaride hili litagubikwa hasa na matukio muhimu yaliyotokea mwaka huu 2015, ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya ugaidi. Kwa mara ya kwanza, vitengo rasmi vya vikosi vya Wizara ya mambo ya ndani vilialikwa kushiriki gwaride hilo. Wawakilishi ishirini na moja wa BRI (kikosi cha kuzima fujo mara moja), wa Raid na wengine kutoka GIGN (polisi ya taifa) watapita mbele jukwaa la rais.

Vitengo hivi vitatu viliendesha operesheni dhidi ya Said na Cherif Kouachi pamoja na Amédy Coulibaly, tarehe 9 Januari mwaka 2015. Watu hawa watatu kwa niaba ya Al-Qaeda katika Peninsula ya Arabia (Aqmi) pamoja na kundi la Islamic State (IS), waliendesha mauaji ya watu 17 ndani ya siku tatu. Itakumbukwa wanahabari na wachoraji wa gazeti la vibonzo la kila wiki la Charlie Hebdo, na mauaji mengine yaliyotokea katika jengo la biashara linalomilikiwa na Myahudi na katika mji wa Montrouge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.