Pata taarifa kuu
UFARANSA-UHISPANIA-NATO-AJALI-USALAMA WA ANGA

Wanajeshi wanane wa Ufaransa wamefariki

Wanajeshi wanane wa Ufaransa na wawili wa Ugiriki wampoteza maisha katika ajali ya ndege ya kivita aina ya F-16 katika kituo cha jeshi la muungano wa nchi za kujihami Nato nchini Uhispania.

Moshi waongezeka kutoka kituo cha mafunzo ya kijeshi katika mji wa Albacete, baada ya ajali ya ndege ya kijeshi yenye ya chapa F-16.
Moshi waongezeka kutoka kituo cha mafunzo ya kijeshi katika mji wa Albacete, baada ya ajali ya ndege ya kijeshi yenye ya chapa F-16. AFP PHOTO / JOSEMA MORENO
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa serikali ya Uhispania Mariano Rajoy amefahamsisha Jumatatu jioni wiki hii kwamba ajali hiyo iliotkea katika mafunzo ya kijeshi dhidi ya wataalamu waliobobea katika kuendesha ndege aina hizo za kijeshi.

Ajali hiyo imetokea mchana wa Jumatatu Januari 26, kulingana na taarifa ya kiongozi huyo wakati wa mafunzo katika kituo cha Nato kwenye umbali wa kilometa 250 kusini mashariki mwa Madrid ambapo kati ya kumi waliopoteza maisha nane ni wafaransa. Taarifa hii imethibithshwa na wizara ya ulinzi ya Ufaransa. Taarifa zaidi zinaeleza kwamba wanajeshi 13 wamejeruhiwa 7 wakiwa katika hali mahtuti.

Kulingana na taarifa iliotolewa na wizara ya ulinzi ya Ufaransa, ajali hiyo ilitokea wakati ndege ya kivita yenye chapa F-16 ya jeshi la ugiriki iliokuwa ikifanya mafunzo na kuanguka muda mfupi baada ya kupaa angani na kugonga ndege nyingi zilizokuwa zimeegesha katika kituo hicho, zikiwemo ndege mbili za Ufaransa aina ya Mirage na nyingine mbili aina ya Rafale ambazo zilikuwa zimepakia mafuta na tayari kupaa angani.

Viongozi wa serikali ya Uhispania wanaeleza kwamba ajali hiyo imefanyika wakati wa mafunzo ya kipekee kwa marubani wenye uzoefu mkubwa wa kuendesha ndege hizo. Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa imefahamisha kwamba chanzo cha ajali hakijajulikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.