Pata taarifa kuu
ULAYA-UFARANSA-UJERUMANI-KUMBUKUMBU-USALAMA

Ulaya yaadhimisha miaka 70 ya mauaji ya Holocaust

François Hollande ametembelea katika eneo kulikojengwa mnara wa Holocaust mjini Paris ili kuongoza sherehe ya kuadhimisha miaka 70 ya kukumbukumbu ya Holocaust.

Sherehe ya maadhimisho ya miaka 70 ya ukombozi wa kambi ya mateso ya Auschwitz, Poland, Januari 27 mwaka 2015.
Sherehe ya maadhimisho ya miaka 70 ya ukombozi wa kambi ya mateso ya Auschwitz, Poland, Januari 27 mwaka 2015. REUTERS/Laszlo Balogh
Matangazo ya kibiashara

Nchini Ujerumani, rais Gauck amezungumza mbele ya Bunge. Hotuba mbalimbali zinatazamiwa kutolewa Jumanne alaasiri wiki hii wakati, wakati wa sherehe katika kambi ya mateso ya Auschwitz, nchini Poland.

Harufu ya jivu. Kambi kubwa, pamoja na mamia kadhaa ya kilomita. Miaka sabini baada ya kambi ya mateso ya Auschwitz, kusini-magharibi mwa Poland, kushuhudiwa ishara ya mauaji ya kimbari ya Wanazi.

Askari wa Jeshi la jekundu, ambaye bado hai ametoa ushuhuda wa kugunduliwa , Januari 27 mwaka 1945, kwa kambi kubwa ya mateso iliyojengwa na Reich ya tatu.

Karibu watu milioni 1.1 waliuawa huko kati ya mwaka 1940 na 1945, ambapo zaidi ya asilimia 90 ya Wayahudi waliuawa. Ili kutosahau kiliyotokea katika enzi hizo, maadhimisho yamefanyika leo duniani kote.

Sherehe zimepangwa kufanyika ndani ya kambi ya mateso ya Auschwitz, wafungwa 300 wa zamani na viongozi wengi wa kimataifa wanatazamiwa kushiriki katika maadhimisho hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.