Pata taarifa kuu
UFARANSA-SHAMBULIO-UGAIDI-MAUAJI

Shambulio dhidi ya Charlie Hebdo, mmoja wa watuhumiwa ajisalimisha

Hati ya kutafutwa kwa watu watatu imetolewa Jumatano Januari 7 jioni baada ya shambulio lililogharimu maisha ya watu 12 na kuwajeruhi wengine 4 kwenye makao makuu ya jarida la vibonzo la Charlie Hebdo.

Picha inayotoa wito kwa mashahidi wa Wizara ya Mambo ya Ndani kuhusu ndugu wawili Kouachi (Charif na Said, kutoka kushoto kwenda kulia), ambao wanatafutwa na polisi kwa uchunguzi kuhusu shambulio dhidi ya makao makuu ya jarida la vibonzo la Charlie Hebdo.
Picha inayotoa wito kwa mashahidi wa Wizara ya Mambo ya Ndani kuhusu ndugu wawili Kouachi (Charif na Said, kutoka kushoto kwenda kulia), ambao wanatafutwa na polisi kwa uchunguzi kuhusu shambulio dhidi ya makao makuu ya jarida la vibonzo la Charlie Hebdo. securité.interieur.gouv.fr
Matangazo ya kibiashara

Mmoja kati ya watuhumiwa watatu amejisalimisha baada ya kujielekeza katika kituo cha polisi cha Charleville-Mézières. Polisi imetoa wito kwa mashahidi.

Mtuhumiwa huyo anaitwa, Hamyd Mourad, mwenye umri wa miaka 18. Hamyd Mourad, ni mmoja wa watuhumiwa mwenye umri mdogo ambao wanatafutwa na vikosi vya usalama baada ya shambulio dhidi ya jarida la vibonzo la Charlie Hebdo.

Kijana huyo mwenye umri mdogo kuliko watuhumiwa wengine wawili amewekwa chini ya ulinzi. Hamyd Mourad alichukua uamzi wa kujisalimisha kwenye kituo cha polisi cha Charleville-Mézières, kaskazini mashariki mwa Ufaransa, baada ya kuona kuwa jina lake limekua likisambazwa nchi nzima na kwenye mitandao mbalimbali.

Hamyd Mourad anashukiwa kuwasaidia watuhumiwa wengine wawili, ambao ni Said Kouachi na Chérif Kouachi. Lakini hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa alihusika katika shambulio lililotokea Jumatano dhidi ya makao makuu ya jarida la vibonzo la Charlie Hebdo.

Watuhumiwa wengine wawili, ambao ni ndugu, mmoja mwenye umri wa miaka 34 na mwengine mwenye umri wa miaka 32 waliozaliwa Paris, na wana uraia wa Ufaransa. watu hao walitimka baada ya tukio hilo na hawajulikanai walipo.

Chérif Kouachi ni mwanajihadi anayejulikana na Idara zinazopambana dhidi ya ugaidi. Alihukumiwa mwaka 2008 kwa kosa la kushiriki katika kundi lililokua likituma wapiganaji wa kiislam nchini Iraq.

Kwa mujibu wa chanzo kiliyo karibu na kesi hiyo kiliyonukuliwa na shirika la habari la Ufaransa AFP, watu kadhaa kutoka familia za watuhumiwa hao watatu, wamewekwa chini ya ulinzi.

Polisi imetoa wito kwa mashahidi, na picha za ndugu hao wawili ambao wanatafutwa na polisi zimewekwa katika maeneo yote nchi nzima na kwenye mitandao mbalimbali.

Watu hawa wawili, Sharif na Said Kouachi ni " kunauwezekano kuwa wana silaha hatari", yameeleza makao makuu ya polisi katika mji wa Paris, na kusema kuwa imetoa "hati ya kutafutwa kwa watu hao wawili ambao ni ndugu".

Mtu yeyote ambaye atakua na taarifa yoyote kuhusiana na watu hao polisi imetoa namba ya simu ambayo hailipwi ukiwa Ufaransa. Namba hiyo ni: 0805 02 17 17.

Serikali ya Ufaransa imeweka siku kuu ya maombolezo ya kitaifa leo Alhamisi Januari 8.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.